Unadhani kwanini unatakiwa kusoma kwa bidii?

Sababu kubwa ni kwamba, itakusaidia kuleta mafanikio ya baadae!

  • Ukweli ni kwamba wakati mwingine maswala ya shule yanaweza kuwa na Changamoto, na inaweza kuwa vigumu kukabiliana na masomo mengi tofauti. Lakini unapaswa kufahamu kuwa, ukiwa na ufahamu mkubwa kuhusu maswala mbalimbali kunakupa wewe nafasi kubwa ya kuzifanikisha ndoto zako.
  • Kama hausomi kwa Sasa, jitahidi kutafuta kozi au mtu atakayeweza kukufundisha ujuzi fulani utakaokufanikisha kuzitimiza malengo yako. Tafuta mtu anayekuvutia kumuiga, mtu anayekuhamasisha, anaweza akawa mwalimu au hata mzazi. Omba msaada na hamasa Kadri unavyozidi kusonga mbele.
  • Lengo ni kile kitu unachokitamani kukitimiza. Ni jambo la muhimu mno kutambua lengo hasa la maisha yako. Hii itakusaidia kujitengenezea mpango wa namna ya kutimiza malengo yako. Tafuta kijitabu kidogo utakachokitumia kuandika malengo na matamanio yako, unaweza kuviandika vitu hivi katika ukurasa mmoja. Na endelea kufuatilia hatua kwa hatua ya utimizwaji wake.
  • Futilia hatua za utimizwaji wake.

  • Jiwekee malengo yatakayokufanya kujikite zaidi kwenye shughuli zako za shule ama mafunzo unayoyafanya. Je unatamani kufaulu? Au kuwa namba moja darasani kwako? Au kuongeza alama zako za ufaulu? Yaandike hayo malengo na yasome Mara kwa Mara.
  • Share your feedback