Jifunze jinsi ya kuwa mwanafunzi bora.
Tunatakiwa kufaulu vizuri darasani, si ndio? Hata hivyo Wakati mwingine, huwa ni vigumu sana kukazana kusoma kwa bidii, lakini kuna hivi hapa vidokezo ambavyo ni vya ukweeli! na rahisi sana vitakavyo kusaidia kuongoza darasani!
Boresha Maisha Yako
Jaribu mfumo huu wa kuandika vidokezo. Ukiwa shuleni, unaweza ukawa unamsikiliza mwalimu wako huku ukirekodi kwa kuandika vidokezo muhimu kutoka katika maelezo yake kwenye kijidaftari chako. Lakini unapofika nyumbani, rejea kuangalia vidokezo vyako tena na urudie kuviandika upya.Hii itakusaidia kuja kukumbuka unachoandika. Unaweza kuboresha muonekano wa vidokezo vyako kwa kuweka manjonjo zaidi iwe kwa kuweka mauwa mazuri, ,au hata vipicha vilivyokatwa na pia kutumia kalamu zenye wino wa rangi tofautitofauti. Ukishapata njia nzuri ambayo itafaa kuremba kazi yako ndivyo utapata motisha zaidi ya kusoma!
Wakati wa Mapumziko
Ipumzishe akili yako kila baada ya lisaa la kujisomea ili ikusaidie kijisikia freshii! Kisha nenda nje utembee kidogo.Hii inaweza kukupa nguvu mpya ya kutulia kuwa makini zaidi.
Simu Yako! Achana nayo kwa muda
Kwasababu tu unaipumzisha akili yako, haimaanishi kuwa unaweza kutumia simu kuchat au kucheza “gemu”. Yaani huu sio wakati wake. Weka mbali simu yako na vifaa vingine vitavyokuvuta uvitumie. Wala sio kwamba eti dunia haitasimama au eti utakuwa rafiki mbaya kwa sababu tuu haujajibu meseji ya besti yako.
Jitathimini
Mwulize ndugu, mzazi au hata rafiki yako (Ni kitu kizuri, kwa sababu nyie ni mashosti na huwa mnasoma pamoja!) kama wanaweza kukutathmini, kwa wao kukuuliza maswali na wewe kutoa majibu.Kwa wewe kukumbuka majibu ya maswali yote wanayo kuuuliza ,hicho ndicho kitakuwa kithibitisho ya kwamba umesoma vya kutosha.
Jipongeze
Swadaktaa kabisaa!!,ukipata maksi za juu kwenye tathmini yako, ni sawa kabisa kujipongeza. Kwa sababu ulifanya kazi nzuri! Inaweza Iwe ni kwa kuingia kwenye facebook yako kwa dakika chache, au kwa kwenda kutembea kwenye maduka makubwa ya nguo yaani wewe tuu kazi kwako!.
Unapaswa kujivunia mafanikio yako!
Share your feedback