Jinsi ya kukabiliana na uonevu mitandaoni.

Mawazo yako (1)

Majukwaa ya mitandao ya kijamii kama vile instagram na facebook yanaweza kuwa mahali panapoleta mzuka wa kujielezea, kuwashirikisha watu wengine mambo yako, mawazo, hisia na kukutana na marafiki kutoka pande zote za dunia. Mitandao hii wakati mwingine inaweza kuwa kama vile rafiki yetu wa karibu sana.

Lakini kuna mambo ambayo wote tunatakiwa kuyafahamu. Jambo la kwanza, mitandao hii ni ya kijamii. Vitu tunavyoviposti na kuwashirikisha wengine mtandaoni vinaweza kuonwa na marafiki zetu, wanafamilia na hata watu tusiofahamiana nao kabisa. Kama hatutakuwa makini tunaweza kuvutia aina fulani ya watu wabaya na hata wale wenye kuonea wengine mtandaoni ambao wanaweza wakawa wanatutukana ama kuandika maoni yanayokera, kuzusha uongo na hata kuwasambazia watu wengine picha zetu bila idhini yetu. Je tutafanya nini ikiwa tutajikuta katika hali ya namna hiyo?

Kuwa mwenye utulivu

Jaribu kupunguza hofu na wala usijibizane. Pale unapopokea ujumbe wa vitisho au wenye chuki achana nao. Kwa kutumia Programu yako ya mitandao ya kijamii unaweza kuiripoti akaunti hiyo lakini pia unaweza kumzuia asiweze tena kuwasiliana na wewe.(Block)Kama unatumia facebook unaweza kubonye sehemu ya picha ya wasifu rafiki huyo kisha upande wa kulia kwa chini kuna vinukta vitatu,ukishabonyeza chagua zuia.Mitandao mingine ya kijamii kama instagram unaweza kufanya hivyo pia.Usisite kumzuia mtu(block)pale utakapojisikia umeonewa.

Kama ilivyo katika maisha ya kawaida, uonevu huwa unafanikiwa pale wanapokuona unakasirika. Na kama ilivyo katika maisha ya kawaida pia jaribu sana kuwapotezea wale wanaokuchukia.

Vunja ukimya ongea na mtu unaemuamini

Kama unamfahamu mtu anayekuonea mtandaoni, unaweza kumweleza rafiki au mtu mzima unayemumini kuhusu hali hii ili aweze kukusaidia. Lakini itakuwa rahisi zaidi kupata msaada kama utaweza kuonyesha uthibitisho wa kile kinachoendelea, hivyo unaweza kupiga picha ya mazungumzo ya meseji alizokutumia au unaweza kuzihifadhi picha hizo katika simu yako ili kudhihirisha kile kinachoendelea.Tunajua hili linaweza kuwa jambo gumu lakini jivunie kwa kupata mtu wa kuzungumza nae, hili litakusaidia katika siku zijazo.

Mara zote unaweza tumia dondoo hizi pale unapohitaji kuzungumza na mtu.

Vuta pumzi ya kutosha

Panga kile unachotaka kukisema

Tafuta sehemu tulivu ili kupata usikivu kutoka kwao.

Ongea ukweli na kwa maelezo ya kina juu ya namna ulivyoonewa.

Ukweli wako utasaidia kuboresha kuleta manadiliko chanya na wenye msaada. Katika tukio kama hilo wengine wanaweza kukulaumu ama kukinzana na wewe, lakini kumbuka sio kosa lako. Hongera kwa kuvunja ukimya, yawezekana hawakuwa watu sahihi, na pale utakapojisikia kuwa upo tayari, jaribu mtu mwingine.

Tumia vizuri programu/ mipangilio ya usiri (Privacy Settings)

Jambo lingine unalotakiwa kukumbuka ni kwamba tunaweza kutumia mipangilio ya usiri tunapokuwa katika majukwaa ya mitandao ya kijamii. Wakati tunapotumia mitandao ya kijamii wakati mwingine huwa tunawashirikisha watu mambo muhimu ya maisha yetu ili kujisikia kuwa karibu na marafiki na ndugu zetu. Lakini taarifa hizi binafsi zinaweza kutumiwa vibaya hasa na wale wanaotaka kutuonea mtandaoni. Tunaweza kupunguza hatari ya uonevu wa mtandaoni kwa kutumia mipangilio ya usiri inayopatikana katika orodha ya mipangilio. Hii inatusaidia:

Kuchagua watu tunaopenda kuwashirikishaa vitu vyetu.

Nani anaweza kuona wasifu wako.

Nanianaweza kuona kile unachokiweka kwenye mitandao.

Ni jambo baya kupitia uonevu wa kimtandao hivyo sote tunaweza kusaidiana ili kuwa salama dhidi waonevu na tuonyeshe upendo kwa kila mtu tuwapo mitandaoni.

    Share your feedback

    Mawazo yako

    Nashukuru Sana! Hongera Kwa Elimu Hii

    Machi 20, 2022, 8:25 p.m