Ushinde msongo wa mawazo (stress)!

Jifunze hapa kupangilia kazi za nyumbani,za shule huku ukijipa raha!

Ukiwa na ratiba ya kazi za nyumbani, kukutana na marafiki zako na kufanya kazi za shuleni, unaweza ukaona kama masaa huwa hayatoshi kabisa.Unamalizaje yale maswali ya hisabati wakati marafiki zako baada kutoka shule wanaenda kwenye ” bethdei” ya Aisha na hapo bado unatakiwa kumsaidia mama yako kuandaa 'Msosi" wa usiku?

Hem vuta pumzi kwanza! kwa sababu tupo kwa ajili yako kukusaidia ili usipate mawazo sana.

Orodhesha: Katika kila mwanzo wa wiki,andaa orodha ya vitu vyote unavyotakiwa kuvifanya kwa wiki hiyo yaani jumuisha: kazi za nyumbani (kama kupika chakula cha usiku na mama yako), vitu vya kujipa raha (kama kwenda kutembea na marafiki zako), na kazi za shule (kama kusoma kwa ajili ya mtihani wa Hisabati)

Ipangilie: Ni vitu gani muhimu zaidi kwenye orodha yako- kipi kinahitajika kufanyika leo na kipi kinaweza kusubiri kikafanyika baadae katika wiki? Kwa kupangilia vitu vyako unavyohitaji kuvifanya,waweza jikuta umebakia na vitu vichache sana vya kufanya katika siku husika .Badala ya kujisikia kuelemewa na mzigo wa kazi nyingi, Vunjavunja ile kazi kubwa kwenye vijikazi vidogovidogo, mfano kazi ya usafi nyumbani waweza ivunja ikawa hivi (Jumatatu –kufuta madirisha, Jumanne-Kufua mapazia,nk)

Jijali: Kwa kujijali, utaweza kutimiza kufanya kazi zilizopo kwenye orodha yako kwa urahisi zaidi. Jipe raha mwenyewe ,mara moja moja sio mbaya kunywa hata angalau ka juisi,chai au hata soda kabla hujaanza kufanya kazi zako za shule. Unapojisikia vizuri ndo vitu huingia kichwani vizuri.

Kuwa Muwazi: Zungumza na wazazi wako pale unapokuwa unajisikia kuelemewa na mzigo wa kazi za shule ulizo nazo. Waelezee kuwa una kazi nyingi za shule, na waombe kama itawezekana iwapo kuna mwenzio hapo nyumbani ashike zamu yako ili uje ushike zamu yake wiki nyingine au ili uje ufanye kazi kubwa zaidi .

Hii pia inawahusu nyie marafiki! Unapotaka ukazurule mchana kutwa wakati unatambua una mtihani unakuja,basi nenda kwa muda mfupi ili uwahi kurudi kujisomea nyumbani,au mnaweza mkasoma pamoja,lakini mmhh!! Kuwa makini tu msije mkaishia kupiga stori tuu.

Share your feedback