Wasichana 500 walishiriki ndoto zao

Hannatu alikuwa mmoja wao

Tulipounda Azimio la Msichana, zaidi ya wasichana wachanga 500 walihojiwa kwenye nchi zote 14. Kisa cha Hannatu kinaakisi changamoto zinazowakabili wasichana wengi tuliozungumza nao...

Elimu, Afya na Uraia

Hannatu msichana mwenye umri wa miaka 12 kutoka Nigeria, anazungumzia kutokuwepo hospitali karibu na pale inapoishi familia yake na usafiri wa karibu sana kuwa ghali zaidi, kinachofanya vigumu kwake kupata huduma ya afya.

Dada na kaka zake wengi wamezaliwa nyumbani na kwa hivyo 'hawajarekodiwa'. Huko ni kumaanisha kuwa hawana vyeti vya kuzaliwa kwa sababu familia yake haiwezi kumudu kuvinunua. Bila cheti cha kuzaliwa hawaruhusiwi kujisajili shuleni.

Vilikuwa visa vya wasichana kama Hannatu vilivyoboresha malengo ya uraia na afya katika Azimio la Msichana, linalowaambia viongozi wa kimataifa kile wasichana wanachohitaji ili kustawi.

Share your feedback