Tujibebe inakusanya taarifa ("data") zinakuhusu ili kukufanya kufurahia zaidi huduma ya Tujibebe na vitu vingine vinavyohusiana na hivyo. Tunapokusanya taarifa zako tunahakikisha zinahifadhiwa kwa usalama na muda wote tunaheshimu sana usiri ( hii ni kwa kipindi chote unapotumia tovuti na hata pale utakapoacha kutumia).
Tumejidhatiti kukupatia usalama na faragha kwa muda wote, tunalazimika kufanya hivi kutokana na sheria mbali mbali zinazotutaka kufanya hivyo ( sheria hizo ni kama zile zinazohusu kulinda taarifa na faragha) sheria hizi zinaihusu taasisi yetu mama ya Girl Effect ( mama wa jamii ya Tujibebe) kwani ofisi zetu zilizopo huko UK
Taarifa tunazokusanya kutoka kwako
Unapojisali ili kuanza kutumia tovuti ya Tujibebe, bila kujali mahali ulipo, tutakusanya na kuhifadhi taarifa fulani zinazokuhusu wewe. Taarifa hizi zinahusisha jina la mtumiaji ( kutokana na uchaguzi wako), umri wako, jinsia yako, neno siri lako, na maswali ya usalama. Kama utashiriki kwa kuchangia mawazo, kupiga kura au kwenye utafiti, ama katika mashindano, Pia tutazitunza taarifa hizo. Lakini pia tunahifadhi jina unalotumia katika mtadao wa Facebook kama sehemu ya taarifa tunazozikusanya.
Taarifa tunazikusanya pale unapotumia tovuti ya Tujibebe.
Unapotumia tovuti ya Tujibebe tutakusanya taarifa za taifa unalotokea na vitu vinavyofanana. Kwa nyongeza kupitia njia zingine za kiufundi kama vile “kuki “tunaweza kukusanya taarifa kuhusu sehemu uliyopo ( kwa mfano kijiji au mji unaotokea). Kuki ni kifaili kidogo kinachopakuliwa kuingia kwenye kompyuta au simu janja yako pale unapotumia tovuti yoyote. Huwa inaruhusu tovuti kutambua kifaa unachokitumia na kuhifadhi baadhi ya taarifa kuhusu vitu unabyopenda na vitu ulivyowahi kuvifanya kwenye tovuti huko nyuma.
Tunatumia “kuki” ili kutambua vitu kama vile ni watu wa ngapi mnaoishinao sehemu moja ambao wametumia tovuti. Kamwe hatutotumia taarifa za mahali ulipo ili kukutafuta mpaka pale tu utakapoombwa kufanya hivyo na ukatupatia kibali.
Pale utakaposhiriki katika upigaji kura na utafiti kutoka Tujibebe tunaweza kukuomba kushikisha taarifa zinakuhusu wewe na maisha yako au kutueleza maoni yako na uzoefu wako. Unaweza kuamua ni taarifa zipi upo tayari kuzishirikisha. Tutazitumia taarifa hizi ili kutusaidia kuhakikisha tunatoa huduma na taarifa bora zenye msaada kwa wanachama wetu wa jamii ya Tujibebe.
Taarifa ambazo utatupatia bila ya sisi kuzihitaji.
Wakati mwingine utahusishwa katika mazungumzo katika jukwaa la Tujibebe au kuhusu huduma zetu zingine. Pale unapotoa maoni yako katika tovuti hii, unaweza kutuma maoni yako bila kutaja jina lako.
Unapokuwa unatoa maoni yako unaweza kutoa taarifa zinazokuhusu kama vile hobi zako, familia, mambo yaliyowahi kukutokea, vitu unavyopenda kuvifanya, mawazo yako pamoja na hisia zako. Mara zote tutajitahidi tunafuatilia maoni haya ili kuhakikisha kwamba vitu vyote visivyo sahihi au vinavyoweza kutumika kukutambulisha tunaviondoa. Tafadhali kumbuka kuwa ni jukumu lako kutokushirikisha taarifa binafsi zinazoweza kukufanya ukatambulika wakati unapotoa maoni yako katika tovuti ya Tujibebe.
Tunatumia taarifa zilizoandikwa katika maoni ili kuelewa mada au stori zipi hupendwa zaidi na watu wanaotumia Tujibebe, na jinsi gani wanachama wa Tujibebe wanavyotumia taarifa zinazoshirikishwa katika jukwaa katika maisha yao ha kila siku, na namna tunabyoweza kuboresha huduma zetu.
Nani tunaweza kumshirikisha kuhusu taarifa zako:
Kundi la kwanza la watu wanaoweza kuona taarifa tulizokusanya kutoka kwako ni watumishi wa Girl Effect ( na wale wanaofanya kazi kwa niaba ya Girl Effect, wote wamesaini makubaliano kwamba watatunza usiri wa taarifa zako na wanatakiwa kufuata miongozo mikali kuhusu usalama na faragha. Watumishi wetu huchaguliwa kwa umakini mkubwa, wanapewa mafunzo, na wanawajibika kwako kama mwanachama wa jamii ya Tujibebe
Kwa nyongeza, wakati mwingine huwa tunashirikiana na makampjni au mawakala wengine ili kutusaidia kuboresha au kusimamia Tujibebe. Watu hawa pia wanaweza kupata mafasi ya kuziona taarifa zako, ingawa kazi yao sio kuzihariri taarifa hizi, wanaruhusiwa kuziona taarifa zako ili kutusaidia kuwafikia watu katika mataifa tunayofanyia kazi.
Kundi hili pia limesaini makubaliano nasi ili kutunza usiri na usalama hii inahusisha vitu wanavyoruhusiwa kufanya na vile wasivyoruhusiwa kufanya juu ya taarifa zako. Lakini kwa mara nyingine tena huwa tupo makini mno kwachagua watu hawa wa kutusaidia.
Watu wengine tunaowashirikisha taarifa zetu wanahusisha:
Washirika wa maudhui. Washirika hawa wanatusaidia katika uandishi wa stori na kudhibiti maoni ya wanachama wa Tujibebe.
Washirika wa taarifa. Tunawashirikisha washirika hawa kuhusu taarifa hizi ili watusaidie kujua kama Tujibebe inafanya kazi vizuri na aina gani ya stori zinapendwa zaidi na jinsi gani tunaweza kuboresha Tujibebe.
Washirika wa teknolojia. Tunawashirikisha washirika hawa wa teknolojia ili wahakikishe Tujibebe inafanyakazi na kitu gani hasa tunaweza kukiongeza.
Washirika wa utafiti. Tunawashirikisha taarifa ili watusaidie kujua kama tovuti yetu imekuwa na msaada kwa watumiaji.
Unaweza kuomba listi ya washirika ambao tunawashirikisha taarifa zetu kama utapenda kufahamu zaidi unaweza kuwasiliana nasi kupitia dataprotection@girleffect.org.
Kama unatumia tovuti yetu au kupitia mtandao wa Facebook or kunasoma tovuti yetu ya Tujibebe kupitia mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Instagram, BBM unapaswa kusoma kuhusu sera zao za faragha ili uweze kufahami jinsi wanavyozitumia taarifa zako
Hazi zako.
Unaweza kutuomba kufuta kabisa taarifa zako tulizonazo, hii inaweza kuwa na maana kwamba hautoweza kutumia huduma zetu tena. Hii inaitwa Haki ya kusahauliwa. Kama hatutokuwa na sababu ya msingi ya kuendelea kuhifadhi taarifa zako tutafurahia kuzifuta. Hata hivyo, kuna wakati tutakapotumia taarifa zako kwa ajili ya takwimu au malengo ya utafiti au kusaidia Girl Effect kufanikisha lengo lake la kuwawezesha wasichina. Kwa sababu kama hizi, hatutoweza kufuta taarifa zako zote, tutaondoa vitu vyote vinavyoweza kukutambulisha ( zile zinazoita taarifa za utambulisho binafsi) na tutahifadhi taarifa zilizobaki kwa ajili ya matumizi yetu zitabaki kama taarifa zisizo na jina ( hii ina maana kwamba haitokuwa rahisi watu kukutambua) Tutakujulisha kama tutafanya hivi. Unaweza kututumia barua pele kupitia dataprotection@girleffect.org Ili kuomba taarifa zako zifutwe au hata kama una maswali kuhusu taarifa zako. Lakini pia unaweza kuomba nakala ya taarifa zinazokuhusu tulibakiza, kama tutakuwa nazo au hata kufanya marekebisho ya taarifa.
Hizi zinaitwa haki zako za kupata na kurekebisha. Tutajitahidi kadri tuwezavyo kujibu maombi yako ndani ya mwezi mmoja baada ya kuhakikisha utambulisho wako. Tafadhali tutumie barua pepe dataprotection@girleffect.org Na tutakutumia fomu ili uijaze ili itusaidie kujua nini hasa ungependa tukifanye.
Malalamiko. Kama haufurahishwi na namna tunavyodhibiti taarifa zako, mara zote unaweza kuwasiliana nasi kupitia dataprotection@girleffect.org Na tutajitahidi kujibu mapema kadri tutakavyoweza ( na mara zote itakuwa ndani ya kipindi cha mwezi mmoja)