Kuweka pesa akiba kuna raha yake. Jaribu kufuata vidokezo hivi vizuri.
Kutenga hela kwa ajili ya akiba huwa ni rahisi sana kusema kuliko kuliko kutenda.Kuna mbinu hapa za kukusaidia katika hilo.
Okoa pesa kwa kutonunua chakula.
Ni kweli unaweza kununua chakula cha mchana au vitafunwa shuleni lakini ukipika nyumbani itakuwa rahisi zaidi na hii ni bora kwa afya yako. Ikiwa unajaribu kuokoa hela zako, kula kabisa nyumbani kabla ya kwenda shule, au kukutana na marafiki zako. Na unapokuwa umeenda kula kwenye hotel flani na rafiki zako basi agiza kinywaji tu au kitafunwa cha bei rahisi,kwa namna hii utakuwa unatumia pesa kidogo tu..
Mtumba ndio uwe mpango mzima kwako!
Usiogope kuvaa nguo za mtumba, kusema kweli nguo za mtumba ndo fasheni,Haswaa kama unajua kuchagua nguo “kali”. Unaweza hata kutafuta zile nguo ambazo dada ,mama yako, au shangazi zako hawazivai tena. Nguo za zamani zinaweza kuwa nzuri sana haswa ukizichanganya na za kisasa,kazi yako ni kuzitengeneza tuu kidogo Jifunze kutumia sindano na uzi au cherahani , pia unaweza kuta kwamba vitu vingi vinahitaji kushonwa kidogo tu ili virudi kuwa vizuri kama zamani.
Jiepushe na tamaa kwa kutopita mitaa ya Madukani,Sokoni au Supamaketi
Unapojaribu kujiwekea akiba, hata kwenda kuangalia vitu dukani bado si kitu kizuri maana utashawishika tuu, haswa ikiwa ni zile nyakati ambazo una usongo wa mawazo, umekasirika au una huzuni huwa tunapenda kununua vitu hovyo hovyo tu . Maana ni kweli ya kwamba watu wengi wakati wamejawa na hisia.hutumia pesa zaidi kwa kununua vitu wasivyovihitaji
Kusanya sarafu (Chenjichenji) ambazo umebakiza
Sisi sote huwa hhatukosi tu miamia au hamsini hamsini katika pochi zetu. Jaribu kuziweka sarafu hizo kwenye chombo fulani kama "kibubu" hivi. Mara watu wanapojua kwamba unakusanya sarafu utashangaa ni watu watakavyopenda kukupa miamia zao. Unapokuwa na sarafu za kutosha, zibadilishe kwa noti katika duka la kubadilisha pesa au zipeleke benki ili usiweze kuzitumia.
Jiepushe na madeni
Kukopa hela kwa ajili ya kujifurahisha inaweza kukufanya ukawa unadaiwa na watu kila kona.Kudaiwa sio kitu kizuri na si hivyo tu, kitendo tu cha kuwa na madeni mengi ni hatari na huleta msongo wa mawazo pia.Kama unaweza basi jiepushe na madeni kwa kufanya matumizi kulingana na mfuko wako.Kama kuna kitu unakitaka basi tunza hela ili uje ukinunue hakika utajisikia mwenye kuridhika bila madeni. Watu wenye madeni yasiyokuwa ya lazima ni nadra "kutoboa "katika maisha – yaepuke na uwe mvumilivu,si unajua subira yavuta heri, na Haba na Haba hujaza kibaba.
Share your feedback