Maswali Mazuri 6 ya kumuuliza mshauri wako

Yafanye maongezi yawe hai

Mawazo yako (19)

Je! Umeshawahi kuanzisha mazungumsho na mtu halafu baada ya dakika 5 tu yakakata kwa sababu uliishiwa maneno? Ndio! Wote tumepitia hii hasa likija swala la kuongea na watu wazima kama wazazi,walezi au washauri.wakati unawaza kuhusiana na hili hakuna haja ya kusikia aibu au wasiwasi kwamba itakuaje.Unahitaji tu kuwa mbunifu katika maswali yako.Kutokujua nini cha kumuuliza mshauri isiwe sababu ya kukosa kutafuta mshauri. Uoga wa kuzungumza na watu ni kitu cha kawaida kila mtu huwa anapitia lakini hii haitakusaidia kuja kuwa mtu uliefanikiwa katika maisha yako ya baadae.

Washauri ni watu wenye ujuzi ambao husaidia kuwaongoza watu wenye ujuzi mdogo katika vitu wanavyovipenda.. Mara nyingi hukufungua akili na kuona mambo kiupana zaidi.

Wanaweza kuleta tofauti kubwa sana katika maisha yako kama utafanyia kazi yale wanayokufundisha katika maisha yako,. Wanasema "Nyota njema huonekana asubuhi" na kuwa na mazungumzo na washauri hulenga hivyo haswaa ! kwa hiyo uliza maswali mazuri yenye maana. Sikiliza vidokezo na “vitu ” vya muhimu wanavyokwambia, halafu vitumie katika maisha yako nawe utajifunza mengi! mengi! na hautabaki kama ulivyo!. si wazo zuri eh?

Ikiwa unapata shida kufanya mazungumzo na mshauri wako, haya hapa maswali mazuri ambayo yataleta msisimko na kuendeleza mazungumzo!

  1. Uliwezaje kupata kazi yako ya sasa?

  2. Ulijifunza vipi jinsi ya kukubali kushindwa?

  3. Je! Kulikuwa na nafasi ya kazi ambayo uliomba na ukapata, lakini haukuwa umekidhi vigezo 100%?

  4. Je, ni nini huwa unazingatia unapofanya maamuzi?

  5. Kwa mtazamo wako, nina uwezo kwenye maeneo yapi, na nafaa kuzingatia nini ili kujiboresha?

  6. Ni maarifa gani mapya ninayohitaji ili nisonge mbele?

Enhee! maswali yapi ungeweka kwenye orodha kwa ajili ya mshauri wako? ushauri wowote wa kutupa sisi? tunaomba utushirikishe kwa kutuandikia hapo sehemu ya maoni.

Share your feedback

Mawazo yako

Nipenda somo lenu kwan linanifundisha nisiyoyajua

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Latest Reply

Samira tunafurahi kwamba makala yetu imekuwa ya manufaa kwako,unaweza kuwambia pia rafiki zako ili na wao wanufaike .Kila la kheri Binti.

Nipenda somo lenu kwan linanifundisha nisiyoyajua

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Nimependa kweli haya maelekezo hakika nitayatumia siku moja.

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Somo zuri mno By culture IV

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Latest Reply

Calture_IV tunashukuru sana kwa kuandika maoni yako,na tunafurahi kwamba umeipenda makala yetu,unaweza kushea na marafiki zako pia.Asante

Ni Kawaida Mtu Kupata Kazi Bila Kukidhi Vigezo Maana Uwezo Wa Mtu Ndio Unamsaidia Kufanya Kazi Aliyoajiliwa Siyo Vigezo

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Latest Reply

Nyangwa, habari. Vipi umeweza kufuatilia dondoo hizi muhimu namna ya kupata taarifa kutoka kwa mshauri wako? Hebu fuatilia na utuambie umejifunza nini?

Ningependa kujiamini ktk kufanya kazi yangu muda wote

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Kama jina naituwa Nobert natoka mji ya busia naogeelea ju ya maisha yangu mm nlkwa na rafiki mpenduwa jina lake ni Quniter anatoka siaya lkn huyo msichana alkwa ananchezea kwa akili ilipo guduwa huyo mrembo anacheza na mm nlmwacha kbxaaaa

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Latest Reply

Jibu ni tuwache kukuwa wauogo

je, umewahi kufukuzwa kazi?

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Binafsi Mimi mwanaume ila Leo kwenye somo hili nimejua jinsi gani yakuendeleza mazungumzo

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

KUSEMA KWELI MI HATA MTUWAKUNISHAUL SINA KWAKWEL NINA WAKAT MGUMU SANA

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Latest Reply

Kama ni kweli unachosema kuwa huna mshauri?? Ni hatari sana ukizingatia wewe ni mtoto wa kike, Mara nyingi huwa ni ngumu kukabili changamoto. Hivyo ni vizuri zaidi kuwa na mtu anayeweza kuwaza badala yako pale unapohitaji msaada huo.

pole dada amina nakuomba tafuta kwenye kikundi hichi ushaur utapata 2

Kupat mushauli ndo nivizul san kwasabab unaweza kushauliwa ndo ukapat unacho kitafuta mazuli san baadae unaweza kupat unacho kiitaji kwajil ya ushauli wako alie kushauli kupata unacho kutafuta ila kwabadae usimuone kama mududu fulani yey ndo alisabisha adi kupata unacho kiitaji ayo ndo maoni yangu et

kupata mushauli nivizu san et kwasababu unaweza kupat ushauli ndo ukapata malenge yako ila simbay et ila kwabadae utapa unacho kitafuta sana ila weng malego yao kuwatimiza ndo unakuta niishu san ila ukiwa na akili yajitegemea itakuwa vizuri ila ushauli ndo muzuli san usijali jamani tuko pamoja sana

Dada YANGU unaishije sasa màana ni ngum