Vidokezo maarufu kwa kipindi chako bora cha kusoma
Kama wengi wetu huenda unapenda kujifunza mambo mapya na kwenda shuleni, lakini unaona changamoto ndogo kusoma kwa ajili ya mitihani na majaribio, sivyo?
Pia unajua kusubiri hadi dakika ya mwisho kutaharibu mambo kabisa. Umechoka kukariri usiku wa kuamkia mtihani? Kwa nini usijaribu vidokezo vipya vya kusoma ili kukusaidia kuwa na mweleko. Vinafanya kazi na vitakusaidia kufuatilia masomo yako.
Panga wakati wa kila mara na eneo la kusomea. Labda ni kwenye meza ya jikoni kila jioni au nyumbani kwa rafiki yako kwa saa moja baada ya kutoka shuleni. Kwa kuweka wakati wa kila mara na eneo, vipindi vyako vya kusoma vitakuwa rahisi kuvifuatilia – na hata kuvifanya kuwa mazoea!
Tenga kazi kubwa kuwa vipande vidogo. Iwe unasomea jaribio kubwa au kufanya mradi, pindi tu unapopata kazi, anza kujipangia mwenyewe malengo madogo ya kila siku. Ukikumbana na kazi kubwa, inakuwa rahisi kulemewa. Pia, kukamilisha malengo madogo kutakuridhisha – na kukusukuma kuendelea.
Pumzika. Ni vyema kujitengea muda unaposoma na kujifunza, unaweza kuzingatia tu kwa muda mrefu kabla ya akili yako haijahitaji kupumzika. Inapendekezwa kupumzika kwa dakika 10 kila baada ya dakika 45 hadi saa 1. Acha vitabu vyako na uende nje kwa dakika chache, zungumza na ndugu zako au andaa chai na mama yako. Lakini usipumzike kwa muda mrefu – la sivyo utapoteza motisha yako.
Tafuta mbinu yako ya kusoma. Watu wengine huona kuandika upya matini (notes) yao ni njia bora ya kujifunza, wengine wanapenda kuongea kuhusu kazi yao kwa sauti na wengine hujifunza vizuri wakiwa na wengine, kushirki maarifa na kusaidiana. Chukua muda fulani kujaribu njia tofauti za kusoma, na utumie ile inayokusaidia. Wakati mwingine huenda ukahitaji mbinu tofauti za kusoma kwa masomo tofauti.
Kila heri, kwa kuzingatia kidogo, unaweza kufanya vyema kwenye jaribio lijalo!
Kumbuka: hata usipokuwa shuleni unaweza kutumia vidokezo hivi kukusaidia kujifunza stadi mpya au kukabiliana na kazi ngumu – jaribu.
Share your feedback