Una haki ya kusoma!

Wasichana kutoka duniani kote wanatambua ya kuwa Elimu husaidia utoke kimaisha!

Kila msichana ana haki ya kusoma na sharti aweze kwenda katika moja ya shule zilizopo karibu naye, na kuwepo na usalama katika kufika hapo. Tunao watu mashuhuri ambao wanakubaliana kabisa nasi (nawe) juu ya hili. Ngoja huu ujumbe wao ukuhamasishe kupambana na masomo shuleni kwakuwa unaweza , maana itaboresha maisha yako ya baadae.

"Hatuwezi kufanikiwa ikiwa nusu yetu hawasongi mbele. Tunawahimiza dada zetu duniani kote wawe wajasiri, Wajikubali kwa uwezo walio nao ndani yao ili wautumie vizuri kwa manufaa yao." Haya ni ya maneno ya Malala Yousafzai, mwanaharakati kutoka Pakistani anayepigania elimu ya wasichana na pia kama mshindi wa Tuzo ya Nobel mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kushinda

"Ishi kana kwamba utakufa kesho. Pambana kijifunza kana kwamba utaishi milele." – Mahatma Gandhi, kiongozi wa vuguvugu lililopigania uhuru nchini India

“Elimu ndiyo silaha kali zaidi unayoweza kuitumia kuubadilisha ulimwengu.” – Nelson Mandela, Rais Mstaafu wa Afrika Kusini na mshindi wa tuzo ya Amani ya Nobel

“Muelimishe mvulana na utakuwa umemuelimisha mtu binafsi. Muelimishe msichana na utakuwa umeielimisha jamii nzima.” – Mithali ya Kiafrika

“Muelimishe msichana, mtambulishe vizuri kwa ulimwengu na mmoja kati ya kumi atakuwa na njia za kuishi vizuri bila kuwa mzigo kwa mtu yeyote.” – EJane Austen, Mwandishi kutoka Uingereza

“Wasichana sharti wafundishwe kuanzia utotoni kwamba wana nguvu na uwezo wa kuwa chochote wanachotaka kuwa. Ni juu yetu kubadilisha takwimu kwa ajili ya wanawake ulimwenguni … na kuwa mfano wa kizazi kijacho cha wasichana.” – Beyonce, Mwanamziki kutoka Marekani na balozi wa masuala ya kibinadamu

“Wasichana wanapoelimishwa nchi zao huwa na uwezo zaidi na zenye mafanikio.” – Michele Obama, mke wa rais wa Marekani

“Sisi ndio mabadiliko tunayoyatafuta. Mabadiliko hayatakuja ikiwa tutasubiri mtu mwingine au tutasubiri wakati mwingine.” – Bipasha Basu, Mwigizaji wa sinema za Kihindi

“Wanawake na wasichana wana haki na nafasi sawa, familia zao, jamii zao na nchi zao hufanikiwa.” – Dr Babatunde Osotimehin, mtaalamu wa afya ya jamii na afisa katika Umoja wa Mataifa kutoka Nigeria

“Wakati wote nimeamini kwamba unapomuelimisha msichana, unaliwezesha taifa.” – Malkia Rania kutoka Jordan

“Ulimwengu hautawahi kutambua asilimia 100% ya malengo yake ikiwa asilimia 50% ya watu wake hawawezi kutambua uwezo wao wote. Tunapowawezesha wanawake kutumia uwezo wao, sisi sote tunajiandalia maisha ya baadaye.” – Ban Ki-moom, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

Share your feedback