Je, unajisikia kukosa mtu wa kuongea nae?

Kuna watu wazima ambao unaweza kuwaamini

Mawazo yako (1)

Wazazi wangu wanaishi katika kijiji kimoja hapa Tanzania. Hali yao ya kifedha haikuwa nzuri, hivyo walishindwa kutuhudumia mimi na kaka zangu wanne,Ikanilazimu mimi nije kuishi huku mjini pamoja na mjomba na shangazi.Nimekuwa nikiishi hapa tangu mwaka jana mwezi wa sita .Kiukweli mara ya kwanza nilipokuja hapa mjini nilikuwa mpweke sana .

Shangazi na mjomba wana watoto wa tatu na wote ni wavulana. Shangazi huwa anasafiri mara kwa mara kufuatilia biashara zake. Kiukweli sikuwahi kupata nafasi ya kuwa karibu nae, nilijisikia mpweke nilipojikuta sina mtu wa kuongea nae. Haswaa pale Nilipoanza hedhi yangu mwezi uliopita, sikujua nimweleze nani.

Kisha nikakutana na Naomi! Yeye alijiunga shuleni kwetu muhula uliopita na tukawa tunakaa wote dawati moja. yaani nilifurahi sana. kwanza yeye ni mtu poa sana halafu ana busara mno. Mimi huwa namwelezea kila kitu. Hata wakati ninapokuwa nina matatizo ya wavulana shuleni huwa namwambia vile vile.

Kwa kuwa sisi ni wa rika moja, Naomi aliniambia sio kila tatizo anaweza kunisaidia. Alisema ninahitaji mtu mzima wa kuwa naongea naye. Aliniambia ninapaswa kuongea na shangazi yangu,Hata kama huwa anasafiri sana haimaanishi hatuwezi kuwa karibu. Aliniambia nijaribu kwanza kuliko kukata tamaa kabisa. Nilikuwa na uwoga kidogo, lakini nikaamua kumweleza shangazi yangu kuhusu jinsi nilivyopata hedhi wiki iliyopita. Huwezi amini alikuwa mwelewa! na isitoshe alinielezea kuhusu kilichokuwa kikitokea mwilini mwangu na hata mambo mengine ambayo Naomi hakuwa anayajua!!

Naomi alinionyesha kwamba hakuna haja ya kuwa muoga kumueleza mtu matatizo yangu. Kwa kawaida watu wazima huwa tayari kusaidia, unachopaswa kufanya ni kuuliza tu! Hata kama shangazi yangu hayupo, sasa ninaweza kuongea na mshauri au mwalimu shuleni kwetu. Nimewapata watu ninaoweza kuwaamini. Wakati mwingine huwa naenda hata kwa binamu yangu Deus kupata ushauri kuhusu wavulana na mara zote hufanya iwe rahisi sana kuyaelewa mambo.

Sasa najua sipaswi kunyamaza ikiwa kuna shida. Ikiwa una tatizo na unahitaji mtu wa kuongea naye, jaribu vidokezo hivi:

Tafuta mtu mzima unayemwamini, kama mama au mwalimu wako.

Fikiria kuhusu unachopaswa kusema na fanyia mazoezi ya kuongea kabla.

Wewe waza tu kwamba kila kitu kitakwenda sawa,Usijipe presha hii itakusaidia kuondoa uwoga!

Kama huna mtu wa kuongea nae wala isikufanye ufikirie sana,Kuna watu wazima kibao ambao unaweza kuwafata ili waweze kukusapoti,mfano Mwalimu,Binamu yako au hata yule mama jirani ambae unaona unaweza kumuamini.

    Watu wazima wana hekima na uzoefu mwingi hivyo wala usione aibu. Wana majibu ya maswali yako!

    Share your feedback

    Mawazo yako

    Mambo

    Machi 20, 2022, 8:25 p.m