Jinsi ya kuweka akiba kwa kushirikiana na Besti yako!

Mnapofanya pamoja, huwa ina raha yake... pia mtapata pesa nyingi zaidi.

Mawazo yako (9)

Hivi majuzi tu, mimi na besti yangu Habiba tulikuwa tunaongelea kuhusu mipango yetu ya maisha. Habiba anataka kuwa mwalimu,mimi nimekuwa nikifiria kuhusu kusomea u Nesi. Tatizo ada ni kubwa mno! Kwa hiyo kwa pamoja tuliamua kuanza kujiwekea akiba kwa ajili ya Ada za shule, limekuwa jambo zuri sana maana:

Tunajaliana.
Tuliamua kuweka akiba pamoja kwa sababu tunaaminiana sana! Mwanzo, tulielezana malengo yetu na kila mtu akaandika kwenye kidaftari chake . Kila wakati tunapotenga pesa za akiba, huwa tunaandika kiwango na tarehe katika madaftari yetu. Hutusaidia kuona jinsi tunavyopiga hatua na inaturahisishia kujulishana maendeleo ya kila mmoja – kitu ambacho tulikubaliana kukifanya kila baada ya wiki mbili.

Tunasaidiana kujizuia/Kuishinda tamaa.
Kuwa na mtu ninaeshirikiana nae katika kuweka akiba humaanisha kuwa hata kama tukienda kula bata na marafiki zetu na wanataka tufanye matanuzi, ni rahisi kujizuia kwa sababu mimi na Habiba huwa letu moja na hata kama asipokuwepo, ninajua baadaye ntampa tu ripoti maana lazima tu ataniuliza, jambo ambalo linaniepusha kufanya matumizi mabaya ya pesa.

Tunajinunulia zawadi za bei chee kwa ajili ya kujipongeza.
Sote wawili tumejiwekea malengo ambayo sio makubwa ya kiasi gani cha hela ambacho tungependa kuweka kama akiba kila mwezi. Tukitimiza tu lengo, tunajipongeza kwa kujipa raha kidogo mfano: huwa twajinunulia "Soda"

Huwa tunatiana Moyo
Hata pale ninapoona kuwa ninashindwa kutimiza lengo langu na kukata tamaa, Huwa namtafuta Habiba na kuongea nae, huwa hunitia moyo nisonge mbele. Kuweka akiba kwa kushirikiana na mtu mwingine husaidia sana kutiana moyo pale tunapoona hatujafikisha malengo na pale tunapofeli.

Tunasaidiana.
Habiba alipohitajika kuhudhuria harusi wikiendi chache zilizopita, alijua kuwa alihitaji nguo mpya, lakini hakutaka kutumia akiba yake. Badala yake, aliomba nimuazime gauni langu lile nilivaa siku ya "Kicheni pati ya Asha" ili alivae siku hiyo. Kwa kusaidiana huku kama kuazimana nguo inatusaidia kuokoa pesa nyingi zaidi.

Share your feedback

Mawazo yako

Ni jambo jema mungu awasaidie

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Nijambo zuri hilo kama mnaaminiana vilivyo

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Latest Reply

Kila laher kwenu

Habari Abaslulu. Asante kwa kufuatilia makala hii. Ni kweli mkiaminiana na best yako mnaweza kufanya mambo haya. Je, unaye rafiki yako unayemwamini kiasi mnaweza kushirikiana kuweka akiba? Je ulishajaribu njia hii? Hebu washirikishe na rafiki zako somo hili nao wajifunze.

Nataka niwe dreva nifanye nini

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Latest Reply

Asante sana Idi kwa kueleza matamanio yako. Je umeweza kufuatilia makala hii namna ya kuweka akiba na rafiki yako? Je makala hii imekusaidia?. Tumeona unatamani kuwa dreva, ni jambo jema. Vipi umejaribu kuchunguza maeneo ya karibu au kuuliza rafiki zako juu ya sehemu na namna unavyoweza kupata mafunzo ya udereva? Hebu jaribu kufanya hivyo kisha uje utuambie.

Nimejifunza kwamba ushirikiano baina yako na rafiki yako huleta mafanikio mengi zaidi kuliko kuwa mwenyw

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

kweli

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Mbinu ya kutimiza ndoto yako

Machi 20, 2022, 8:25 p.m