Jitafutie marafiki wazuri – katika ulimwengu halisia

Je, una marafiki wengi mtandaoni kuliko wale unaowajua ana kwa ana? Jifunze kujenga mahusiano halisi leo.

Simu yako ya mkononi, intaneti, kompyuta – ni vitu vizuri sana! Unaweza kukutana na watu wapya, kujifunza mambo mapya na kushiriki mawazo na marafiki kutoka duniani kote. Lakini vipi kuhusu wale marafiki wanaoishi mtaani kwako? Intaneti ni nzuri lakini ikiwa kuwako kwako kwenye mtandao kumeleta kizuizi kati yako na marafiki zako wa kweli, huenda wakati umefika wa kuweka simu chini na kuujua ulmwengu bila #kichujio chochote!

Mazungumzo halisi

Ammera, mwanafunzi wa shule ya sekondari mwenye umri wa miaka 16, alituambia kuhusu kipindi alipoenda sehemu anayoipenda siku ya Jumamosi. Marafiki zake wote walikuwa huko, lakini palikuwa na kimya kingi isipokuwa milio ya simu iliyotoka kwenye simu zao. Hali ilianza kuwa ya kushangaza zaidi wakati mmoja wa marafiki zake wakubwa, aliyekuwa ameketi karibu naye alipomtumia SMS!

Huo unaweza kuonekana kuwa ni ujinga, lakini ni kitu ambacho wengi wetu wamewahi kukipitia. Ikiwa umechoka kuhisi kana kwamba uko peke yako hata unapokuwa na marafiki zako, hapa kuna wazo la kukusaidia – amua kuweka azimio kwamba mtu wa kwanza kutumia simu yake wakati mko pamoja anawaimbia watu wote wimbo wa kipuuzi au anafanya kitu cha kumwaibisha. Ikiwa hilo halisaidii kuwafanya marafiki zako waweke simu chini, basi hakuna kitakachoweza kuwazuia.

Ulimwengu halisia

Tunapenda intaneti– kuna mengi sana ya kujifunza na kufanya na kufikiria juu ya mtandao. Unapoishiwa na mambo ya kuperuzi kwenye Google, kuna zile picha za kuchekesha za paka!

Usisahau yale yaliyo muhimu sana: watu walio karibu nawe. Marafiki zako. Familia yako. Wale unaowajali. Hakikisha upo katika maisha yako ili uwe na vitu vya 'kupenda' na 'kushiriki' katika ulimwengu ulio halisia.

Share your feedback