Unachohitaji kujua
Huenda ukawa mgeni kwenye haya mambo ya mitandao – labda ndio kwanza umepata simu mpya, au ndio umeanza kutumia mara moja moja ile ya dada yako. Ama ndio kwanza umefungua akaunti kwenye mitandao ya kijamii. Dunia nzima iko kwenye Intaneti - lakini kama ilivyo katika dunia halisi, kuwa humo kunaweza kukuletea faida na hatari pia.
Intaneti ina mambo mazuri sana ,inakupa fursa ya kukutana na marafiki wapya facebook, na kuwapata wale mliopotezana , ila pia kupitia “google “ unapata taarifa kuhusu mambo mengi mapya, kupata msaada kwa mazoezi ya shule au kutafuta matangazo ya kazi.Lakini ni muhimu kufahamu hatari unazoweza kukumbana nazo ukiwa mtandaoni, na kujua jinsi ya kukabiliana nazo.
Baadhi ya hatari unazoweza kukumbana nazo mtandaoni ni pamoja na:
-Uonevu wa mtandaoni - kama vile posti, maoni au meseji za kukera,kukwaza na hata za kukutishia usalama wako.
-kupata makala zisizofaa kama vile picha za ngono au za ukatili
-waporaji wa mtandaoni - kwa maneno mengine, hawa ni watu wazima wanaotumia intaneti kujaribu kuwasilina kwa kuchat na watoto au wasichana kama wewe tu. Nia zao huenda zikawa za kudhuru, kukuonea au kuwa na uhusiano kwa faida zao binafsi - kuposti taarifa nyingi za binafsi au za siri, ambazo zinaweza kukutia wewe, marafiki na familia yako hatarini.
Tunataka uwe salama kadri inavyowezekana wakati wowote na popote unapotumia mtandao.hivi hapa vidokezo vya namna ya kuwa salama mtandaoni.
Kuwa na makini na watu unaochati nao.
Kama kuna mtu kakutumia urafiki na wewe humjui, usikubali na futa kabisa ombi lake.
Usiweke wazi au kumpatia mtu yeyote usiemjua taarifa zinazokuhusu kama anuani yako, au namba ya simu..
Kuwa makini na kile unachoposti mitandaoni.
Unapochagua picha ya kuweka kwenye wasifu wako(profile) kwenye mitandao ya kijamii kama facebook epuka kuchagua picha ambayo itampa mtu kujua wapi unaishi.
Fikiria mara mbili mbili juu ya kile unachoposti kipi kionekane kwa watu wote na kipi wasione.
Hakikisha kwenye simu yako kitufe cha kutambua eneo(location) kimezimwa,kwa ajili ya kulinda usiri maana kuna wavuti au "Apps" ambazo hujulisha watumiaji wengine mahali ulipo pasipo wewe kujua.
Usiposti vitu kama anuani yako au namba ya simu mitandaoni
Usifungue au kupakua "Apps" zinazokuwa zikijitokeza kwenye screen yako kama huna uhakika nazo kwani zinaweza kukuletea vitu visivyofaa.
Usimuonyeshe mtu neno siri lako, na unapotumia simu ya mtu mwingine ili kuingia kwenye akaunti zako za mitandao ya kijamii, unapomaliza hakikisha unabonyeza kitufe cha "Toka nje" au "log out"
Share your feedback
Mawazo yako
Nataka picha za ngono
Machi 20, 2022, 8:25 p.m
Habariyako
Machi 20, 2022, 8:25 p.m
🙏🙏🙏asante
Machi 20, 2022, 8:25 p.m
Asante Sana!
Machi 20, 2022, 8:25 p.m