Mbinu 4 za kupata kile unachokitaka

Jinsi unavyoweza kuongea na wazazi wako na wakakusikiliza.

Mawazo yako (13)

Sote tuliwahi kupitia huo mtihani - wakati unapotaka wazazi wako wakupe "sapoti" kwenye jambo lako fulani halafu hata hujui wapi pa kuanzia kuwaelezea. Inaweza kuogopesha "kinoma!"

Ila waala hakuna haja ya kuwa na wasiwasi.... kwa kweli wazazi wanaweza kuwa msaada mkubwa sana kukuwezesha kutimiza ndoto zako. Unapaswa tu kujua namna nzuri ya kuongea nao!

Ikiwa unajisikia kama uko tayari kujaribu basi - hapa kuna baadhi ya vidokezo vya kukusaidia kupata msaada unaouhitaji kutoka kwa watu wanaokujali!

1. Ongea nao kwa heshima na kwa kuwaonyesha ya kuwa unawathamini

Ni muhimu kuwanyesha hili wakati unapohitaji msaada wao. Itaonyesha kwamba unatambua thamani yao kwako na wafurahia na kushukuru kwa yale yote waliyokufanyia.

Kwa mfano, Waweza kusema "Baba na Mama, ninajua mko "bize" sana lakini mkipata nafasi, naomba mnisaidie kwenda kuninunulia madaftari mengine"

Kuwaonyesha ya kuwa unawaheshimu na kuwajali kunaweza kusaidia sana katika kuwashawishi wafanye yale unayoyataka..

2. Kufanya utafiti muhimu

Mojawapo ya njia rahisi za kuwasaidia wazazi wako kuelewa kwa nini unahitaji wakusaidie ni kuwa na maelezo yenye maana. Wakati unapotafuta maelezo ya kuwambia kumbuka:

Kuandika pointi zako.

"Jitahidi kunyoosha maelezo" ili kuhakikisha unaeleweka.

Watolee mifano ili uwashawishi wakusapoti kile unachokiomba.

Wasikilize wazazi wako, huenda wakawa na maoni au maswali pia kwa hiyo mpeane nafasi ili kila mtu aseme yake.

  Kwa mfano, ikiwa unatafuta kuanzisha biashara, ongea na wazazi kuhusu ni kwanini unadhani hilo ni wazo zuri na uwaonyeshe ya kuwa upo tayari kupokea ushauri wao.

  3. Kuwa tayari kwa lolote,na uwe muwazi

  Iwapo utaona mazungumzo hayaendi jinsi ulivyotarajia ni muhimu sana wewe kutulia tu. Sio kila siku maombi yako yatakubaliwa kwa hiyo ni kuvumilia na kusubiri. Iwapo wazazi wako watakukatalia basi wewe kubali tu, unaweza kuwauliza maswali na watakujibu ili uweze kuelewa.

  Watafurahi kwamba unawasikiliza na kuheshimu mawazo yao,ila hii itakupa nafasi ya wewe kufikiria njia nyingine ya kuwaelezea kile unachokihitaji.

  4. Wahusishe katika kila hatua

  Unaweza kupendekeza kwa kuwaeleza kwamba utakuwa unawashirikisha katika kila hatua ya kile ambacho wamekukubalia

  Kwa njia hii, wataona kwamba,hakika unataka wawe sehemu ya kufanya maamuzi kuhusu jambo lako. Lakini Mwisho hii ni njia nzuri ya kujenga uaminifu na watu wako wa karibu,na itakusaidia hata katika mahusiano yako yoyote huko baadae.

  Share your feedback

  Mawazo yako

  Jee? Kama Mzazi hukupendi au ni mzazi wa kambo

  Machi 20, 2022, 8:25 p.m

  Latest Reply

  Kreddauh tunashukuru sana kwa kuandika maoni yako.Je umejaribu kutumia kati ya hivi vidokezo vilivyopo katika makala hii? tunaamini vitakuwa vya msaada kwako.Hebu jaribu kisha waweza kuja kutushirikisha jinsi ilivyokuwa.Tungefurahi sana kusikia tena kutoka kwako.Asante

  Kwangu Mm Bado Napata Wakati Mgumu Mana Wazazi Wangu Wako Bize Sana Me Nasoma Niko Kidato Cha Pili Lakin Hata Siku Moja Mzazi Wang Hajawahi Kugusa Hata Daftar Langu Hii Inanikatisha Tamaa Sana

  Machi 20, 2022, 8:25 p.m

  Latest Reply

  Mapigo Asante sana kwa kuwa na ujasiri wa kutushirikisha hali unayoipitia.Je una mtu mwingine yeyote unae muamini ambae unaweza kumshirikisha, kama vile Mjomba,shangazi,Kaka au dada? tunaamini kwa kupata mtu unaemuamini anaweza kuwa mshauri mzuri wa kukutia moyo,lakini pia unaweza kujaribu vidokezo vilivyopo katika makala hii kisha waweza kuja kutushirikisha tena kama kama vimekuwa vya manufaa kwako.Wana Tujibebe tungependa kusikia tena kutoka kwako.Kila la kheri

  Hakuna kosa yote yako sahihi piah nsdhukulu nmeelewa na,nmelimika

  Machi 20, 2022, 8:25 p.m

  Latest Reply

  Tunashukuru sana Anoddy kwa kuandika maoni yako na Tunafurahi ya kuwa makala hii imekuwa ya manufaa kwako.Unaweza kusoma makala zingine ili kujifunza zaidi.

  Anoddy Tunafurahi kuona makala zetu zinakuwa za manufaa kwako.Unaweza kuwambia na rafiki zako pia kuhusu makala hizi.Asante

  Mimi Napitia Wakati Mgumu Kwani Nilitamani Mzazi Wangu Awe Wakwanza Katika Kunisaidia Kutatua Changamoto Ila Naona Kabisa Nikiwa Nakandamizwa Kimawazo Nakuchangia Kufelisha Ndoto Zangu

  Machi 20, 2022, 8:25 p.m

  Mimi Napitia Wakati Mgumu Kwani Nilitamani Mzazi Wangu Awe Wakwanza Katika Kunisaidia Kutatua Changamoto Ila Naona Kabisa Nikiwa Nakandamizwa Kimawazo Nakuchangia Kufelisha Ndoto Zangu

  Machi 20, 2022, 8:25 p.m

  Thankx a lot👍💖💖💗💗💝💝😁😀😊

  Machi 20, 2022, 8:25 p.m

  Nadhan ni vzri kuzingatia muda wa kuongea nao pmj na mood zao sio mzaz yupo ktka mawazo yake mengine ukamiongezea na yako😊😊

  Machi 20, 2022, 8:25 p.m

  Mimi ajitaid kuweka malengo ninapo kalibia kufkisha kile kiwango juu ya ile lengo huwa unakuta nabadili uamzi nakufanya kitu kingine naimbeni ushauli wenu nifanyeje?

  Machi 20, 2022, 8:25 p.m

  Nahitaji uxhilikiano

  Machi 20, 2022, 8:25 p.m