Je Kuposti picha nyingi ni Sawa ama Si sawa?

Kuwa makini na hizi hatari zake.

Mawazo yako (3)

Unaweza ukashangaa, kwamba inawezekanaje kuposti picha tu kwenye mtandao iwe jambo la kulihofia? Lakini Tujibebe ipo hapa kukwambia kwamba tunapaswa kuwa makini kuhusu vitu tunavyoviposti mitandaoni kwani kadri teknolojia inavyozidi kuwa bora zaidi, huwapa urahisi zaidi wale wanaotaka kufahamu mengi kuhusu sisi kutujua kwa kupitia picha moja tu.

Labda tuseme unaposti picha uliojipiga ukiwa na rafiki yako ukiwa shuleni au nyumbani kwenu. Mtu yoyote anayeiona hiyo picha anaweza kujua shule unayosoma au mahali unapoishi. Hivyo huwa ni rahisi kujua mahali ulipo. Kama hautozima " kitufe kinachosema mahali ulipo" katika programu ya mipangilio ( programu hii huwa inakuwezesha kuwashirikisha wengine mahali ulipo ama huduma nyinginezo) na wanaweza kutambua haswaa hata eneo ambapo ulipigia picha.

Hivyo tunapaswa kuwa makini na aina ya picha tunazopiga na taarifa zetu binafsi tunazowashirikisha watu mtandaoni.

Na ili tubakie salama ni jambo zuri sana kama tutazima kitufe cha programu inayoeleza mahali tulipo katika simu zetu na katika mitandao ya kijamii tunayoitumia, kama vile facebook, instagram, au twitter. Na kama hatuna uhakika ni bora hata tusiposti kitu.

Kumbuka unapokuwa ukijivinjari mtandaoni ni vyema ukajitahidi mara zote kuwa salama

Share your feedback

Mawazo yako

Kweli kabisa thanks

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Latest Reply

Sana kwa maana teknolojia inakuwa

Vizuri

Machi 20, 2022, 8:25 p.m