Msaada! Akaunti yangu ya Facebook ilivamiwa!(ilidukuliwa)

Ninalitatuaje hili?

Akaunti yangu ya Facebook inatuma meseji za ajabu na sijui ni kwa nini. Inatuma vitu ambavyo hata mimi sijaidhinisha. Marafiki zangu wanasema kuwa akaunti yangu imevamiwa. Ninawezaje kuzuia jambo hili?

Wako Mwaminifu,

Mwenye wenye Huzuni aliyevamiwa

Mpendwa Mwenye huzuni,Uliyevamiwa

Ooh , Jamani inaonekana kama akaunti yako ilivamiwa. Kwa maneno mengine, mtu ameingia katika akaunti yako na anaposti kwa niaba yako, akijifanya kuwa wewe. Wakati mwingine hili hutokea ukisahau kujiondoa kutoka kwenye akaunti yako unapokuwa kwenye Kituo cha huduma ya mtandao kwa kulipia(intaneti kefu). Pia linaweza kutokea ukiruhusu rafiki yako kuomba simu yako ya mkononi. Wakati mwingine ni wavamizi watalaam tu wanaoweza kuingia katika akaunti nyingi kwa kutumia mbinu za hali ya juu sana.

Wavamizi (wawe marafiki au watu usiowajua) hu posti kutoka kwenye ukurasa au akaunti yako pasipo wewe kudhibiti. Wakati mwingine marafiki hufanya jambo hili kama utani, lakini ni muhimu kujaribu kupata udhibiti wa akaunti yako haraka uwezavyo!

Kwenye tovuti nyingi za mitandao ya jamii kama Facebook na Twitter unaweza kuripoti akaunti yako ikiwa imevamiwa. Ikiwa ilifanywa na marafiki wanaofanya mzaha, badilisha tu neno lako la siri hilo pia linaweza kutatua tatizo.

Kila mara kumbuka kuondoka kwenye akaunti na utunze nenosiri lako salama, iwe unaingia katika akaunti kwenye Kituo cha huduma ya mtandao kwa kulipia au simu ya mkononi ya rafiki. Huenda ikaonekana kutokuwa muhimu, lakini inaweza kukulinda dhidi ya mtu anayechapisha vitu kwa niaba yako vinavyoweza kukuaibisha au kukuchafulia jina lako.

Kila la heri unapotatua tatizo la uvamizi!

Akupendae

Bi Nai

Share your feedback