Hebu Jipime kwa hili jaribio letu kujua wewe ni aina gani ya mwekaji akiba wa pesa.
Jibu maswali haya manane kujipima kama wewe ni mwana matumizi mzuri wa pesa – au u mwekaji bora wa akiba.
1. Kama umepewa sasa hivi kiasi cha pesa na ndugu yako...
A) Fastaa! unaenda kununua kitu ambacho umekitamani. B) Utaziweka kwenye akaunti yako ya benki,Kibubu au kuziweka mbali mahali salama kwa ajili ya maisha yako ya baadae.
2.Uko sokoni na una pesa ambazo umekuwa ukijiwekea akiba mwezi huu, Mara umeona nguo flani za ukweIi! halafu zinauzwa kwa bei nzuri Utafanya nini?
A) Utalinunua. Isitoshe, akiba huwa zinawekwa ili zitumike! B) Utambembeleza mwenye duka akupunguzie tena bei.
3.Wewe hufanya maamuzi kuhusu matumizi ya pesa kulingana na...
A) Hisia zako. Yaan wewe ni wale wa "ukiwa na huna raha fanya kile moyo unataka,yani raha Jipe mwenyewe .. B) Mipango uliyoweka ya jinsi unavyotaka kutumia pesa maishani mwako
4.Kwako, pesa inamaanisha...
A) Kujipa raha na starehe B) Kuwa na maisha bora ya baadaye.
5.Je marafiki au wanafamilia huwa wanakudai pesa mara kwa mara?
A) Mara nyingi – Kukopa kitu cha kawaida sana.Hata matajiri mbona wana madeni. B) Sio mara nyingi – Sipendi kudaiwa pesa na watu.
6.Je, huwa unafuatilia jinsi unavyotumia pesa zako, kwa kuandika manunuzi au kutunza risiti?
A) Hapana B) Ndiyo.
7.Kipi ungependa kufanya
A) Matumizi kwanza, akiba baadaye. B) Kuweka akiba sasa, Matumizi baadaye.
Sasa jumlisha ni mara ngapi ulijibu A na ni mara ngapi ulijibu B.
Share your feedback
Mawazo yako
b a
Machi 20, 2022, 8:25 p.m
Latest Reply
Wambula,asante kuandika maoni yako,je umeweza kubofya ili kuona majibu yako?
Wambula,asante kwa kuandika maoni yako,je umeweza kubofya ili kuona majibu yako? Tunatumaini makala hii imekuwa ya manufaa kwako.Asante