Sasa jumlisha ni mara ngapi ulijibu A na ni mara ngapi ulijibu B. Bofya hapa uone majibu yako
Kama majibu yako mengi yatakuwa A basi wewe ni mmoja kati ya watu ambao wana matumizi mabaya ya pesa.
Hata pale ambapo sio vibaya kujipa raha mwenyewe siku moja moja lakini unapojitahidi kutunza pesa kutakusaidia kufanya mambo makubwa zaidi baadae. Kama huwa inakuwia vigumu kutokutumia pesa basi unaweza kuacha mkoba/pochi yako nyumbani pale unapokwenda kwenye mtoko. Unaweza pia kuwaomba wazazi, mlezi au hata mtu unayemuamini ili akusaidie kutunza pesa za akiba hata ikiwa ni kwa kukusaidia kufungua akaunti ya benki au kukutengenezea kibubu hakikisha tu kiwe na kufuli ili uweze kutunza pesa zako nyumbani kwa usalama.
Kama majibu yako mengi ni B basi wewe ni mmoja kati ya watunzaji pesa wazuri kwa ajili ya akiba.
Wewe una mipango mikubwa na unapoweka kwa sasa pesa hizi za akiba itakusaidia kuyatimiza malengo yako hapo baadae katika maisha yako.Je umefikia malengo yako katika utunzaji pesa kama akiba? Je umefanikiwa kutunza pesa kila wiki kwa miezi mitatu mfululizo bila kuzitumia? Kama umefanya hivyo unaweza kujipongeza kwa kujifanyia kitu kidogo. Hii itakuhamasisha zaidi kuendelea kutunza pesa kwa ajili ya mambo makubwa, kama vile yanayohusu elimu au kuanzisha biashara
Kama idadi ya majibu yako uliyojibu A yanalingana na yale uliyojibu B basi wewe ni wa wastani
Upo wastani. Huwa unajitahidi kutunza pesa lakini pia unapenda kula bata na hivyo wakati mwingine huwa unalazimika kutumia pesa zaidi ya unavyopaswa. Weka kumbukumbu ya matumizi ya pesa zako hii inaweza kukusaidia kutunza pesa zaidi. Kila mwanzo wa wiki andika kiasi cha pesa ulichonacho. Halafu kila unapotumia pesa, andika katika kijidaftari chako na elezea ulitumia pesa hiyo kufanyia nini. Mwisho wa mwezi utajionea wapi hasa pesa zako hutumika zaidi na kwa jinsi gani unaweza kujiwekea akiba zaidi. .
Share your feedback