Ni kweli kwamba hedhi inaweza kusababisha maumivu, lakini hii haimaanishi kuwa hedhi zote zitakuwa hivyo. Nataka nikueleze dondoo chache zitakazokusaidia...
Kila msichana hupitia katika kipindi kama hiki kila mwezi, yani namaanisha kuwa katika siku zako za hedhi. Hii ni Hali ya asili katika ukuaji hivyo haipaswi kuwa kitu kibaya.
Kuondoa maumivu
Kama utapata maumivu makali ya tumbo kabla ama wakati unapokuwa kwenye hedhi, tambua haupo pekee yako. Wasichana walio wengi hupata maumivu ya tumbo na mgongo, hii hutokana na ukweli kwamba misuli katika tumbo lako la uzazi (uterasi) hufanya kitendo cha kuondoa ukuta wa ndani wa tumbo lako la uzazi. Na unaweza ukaona labda hutakiwi kutoka nje kwenda kucheza na marafiki zako unapokuwa kwenye hedhi--hii sio kweli. Mazoezi ni njia nzuri sana ya kukusaidia kupunguza maumivu ya tumbo. Hakikisha unatumia pedi au kitambaa kisafi ili kukinga damu na unapaswa kubadili Mara kwa mara ili kuzuia usipate maambukizi ya bakteria.
Njia nyingine ya kupunguza maumivu ni kwa kuoga maji ya moto au kukumbatia chupa ya maji moto iliyoviringishwa kwenye nguo au taulo na kuiweka katika tumbo. Habari njema ni kwamba maumivu haya hayapaswi kuzidi ndani ya siku moja ama mbili.
Mihemuko ya hisia
Je umewahi kulia kwa sababu ya kitu kidogo tu ambacho mama au baba yako alikisema? Je ulimnunia shoga ako kipenzi na bila hata sababu ya maana na hukumbuki kwanini ulifanya hivyo? Hii ni Hali ya kawaida kabisa. Homoni ambazo ni kama wajumbe wanaotembea kwenye damu na kutuma taarifa sehemu mbalimbali za mwili wako ndizo ambazo huhusika na mzunguko wako wa hedhi na ndizo zinazopaswa kulaumiwa.Kadri zinavyopanda na kushuka ndivyo ambavyo hisia zako huwa kuna wakati utakuwa na mihemuko mikali kuhusu mambo madogo madogo. Kuwa hivi haimaanishi kwamba una tatizo lolote,hali hii ni ya kawaida kabisa, ila pale unapokuwa na uelewa inakuwa rahisi zaidi kujizuia.
Kushambuliwa na chunusi
Utagundua kuwa siku chache kabla hujapata hedhi,hata kama huwa hauna chunusi katika hali ya kawaida. chunusi hutokea usoni Kwa mara nyingine unaweza kuzilaumu homoni zako. Lakini wewe kunywa maji mengi, yatausaidia mwili wako kuondoa sumu na kuondoa bakteria wanaosababisha chunusi. Na hakikisha hauli vyakula vya mafuta, vinywaji vya viwandani, na vitu vya sukari, hivi husababisha chunusi kujaa usoni.
Jinsi unavyoweza kujua kama kuna kitu hakipo sawa
Maumivu ya tumbo, mihemuko ya hisia na chunusi usoni, zote ni dalili za kawaida upatapo hedhi. Lakini kuna baadhi ya vitu ambavyo sio vya kawaida. Kama mwili wako utaonyesha dalili zozote Kati ya hizi zifuatavyo hakikisha unamuona daktari, mtaalamu wa afya au nenda katika kliniki iliyopo jirani.
Share your feedback