Mambo ya Kufanya na Kutofanya ili kuondoa chunusi

Jinsi ya kupata ngozi yako laini

Kipindi cha kubalehe ni wakati wa kusisimua wenye mabadiliko mengi yanayotokea mwilini mwako. Kwa bahati mbaya uso wako unahusika katika mchakato wa mabadiliko na unaweza kupata 'marafiki' madoadoa kwenye mwili wako uliokuwa laini awali.

Hiyo ndiyo habari mbaya. Habari njema ni kuwa usaidizi upo hapa!

Wakati wa mzunguko wako wa hedhi, viwango vya homoni zako hupanda na kushuka kwa viwango vikubwa. Homoni ni chembe ndogo za usafirishaji katika mfumo wako wa damu zinazotuma miitikio ya kemikali katika sehemu mbalimbali za mwili wako. Homoni huathiri tezi zako za mafuta, ambazo huongeza utendaji na kuzalisha mafuta zaidi yanayofanya ngozi yako kuwa nyororo. Mara nyingi hii husababisha viini kunaswa na hatimaye kusababisha chunusi. Yote hayo ni sehemu ya kukua na hakuna haja ya kujihisi vibaya au kuaibika – humtokea kila mtu. Lakini kuna mambo machache ya kufanya na kutofanya yanayoweza kukusaidia kuzidhibiti.

Usitoboe!

Ndiyo, kila mtu hujaribiwa, lakini hii hapa ni sababu hupaswi kutoboa chunusi. Kutoboa chunusi kunaweza kusukuma uchafu zaidi katika ngozi yako, hivyo kusababisha kuvimba, wekundu na hata kovu! Ikiwa unajaribu kusuluhisha tatizo na unatarajia kuenda kutembea na marafiki, oga kwa maji moto au tia mvuke usoni mwako kwa kumwaga maji ya moto kwenye bakuli, funika kichwa chako kwa taulo kisha uinamishe kichwa chako kwenye bakuli ukinasa mvuke wa moto (hakikisha hukaribii maji, la sivyo utaungua). Mvuke utasaidia kufungua vinyweleo na kichwa cha chunusi kuweza kulegea.

Dumisha usafi!

Osha uso wako asubuhi na usiku kwa maji vuguvugu na sabuni laini. Usisugue – ngozi yako itakwaruzika. Na usisahau kuilainisha. Jaribu mafuta ya nazi, ni kilainishi bora cha asili.

Usiguse!

Ni vigumu lakini jaribu kutogusa uso wako kwa vidole vyako. Bakteria au viini vyovyote kwenye vidole vyako vinaweza kuambukiza ngozi yako. Hakikisha kuwa umenawa mikono yako kabla ya kujipaka marashi au mafuta usoni.

Fua nguo zako!

Unavalia miwani? Una simu ya mkononi? Hakikisha ni safi ili kuzuia uchafu wowote kukwama kwenye ngozi karibu na macho, pua na chini ya taya.

Kunywa maji!

Maji safi ni njia bora ya kuondoa sumu katika mwili zinazoweza kusababisha chunusi. Isitoshe, maji pia husaidia kulainisha ngozi na kuifanya yenye afya kwa miaka mingi. Kunywa maji glasi moja jambo la kwanza asubuhi na uweke mengine ndani ya chupa karibu nawe ili unywe siku nzima.

Share your feedback