Je! Kuwa kwenye siku zako inabidi iwe siri?

Walaa sio kitu cha kuonea aibu.

Kuvunja ungo kwa mara ya kwanza huwa ni bonge ya changamoto!

Utapata mabadiliko ya hisia mbalimbali kwa wakati mmoja – Uoga,furaha,kuchanganyikiwa,kujisikia kudhalilika,na hakika utakua na maswali mengi.

Walaa hata usichoshwe na hizi hisia zote na kuwaza kwa kuogopa watu watasema nini.kumbuka kila msichana lazima avunje ungo na kupata hedhi ni hali ya kawaida sana na njia ya kumudu hali hii ni kuiongelea tuu!

Jinsi ya kuwambia marafiki zako

Kama marafiki zako hawawezi ongea kwa uwazi kuhusu mtu kuwa kwenye siku zake na mambo yanayohusiana na hedhi basi ni wakati wakuzungumza sasa.Kama huwa unatumia muda mwingi na wasichana pamoja na wavulana basi jaribu kutafuta muda ambao mtakuwa wasichana tu halafu anzisha mada kuhusu hedhi.Mfano unaweza kuanza kwa kusema hivi “Nimeona siku zangu mwezi huu nna furaha hatareeee” vipi wenzangu kuna yeyote alieona siku zake??? ukweli wako ndio utakaowashawishi marafiki zako kufunguka na utashangaa kua wewe sio wa kwanza kwenye kikundi chako kuanza kupata siku zako. Kikubwa kuhusu kuwa wazi kati yenu ni kwamba mtaweza kusaidiana kwa mawazo na kupata majibu ya maswali kuhusu kuona siku zenu.

Jinsi gani utawambia familia yako?

Unaweza kua unaishi na mama tu au wazazi wako wote au baba tu au hata shangazi.Haijalishi familia gani unatokea ni muhimu kuwajulisha walio karibu yako nini kimetokea kwako.Hii itawapa nafasi ya kukusaidia na kukununulia mahitaji ya muhimu unayohitaji kipindi cha hedhi kama pedi nk. Tafuta muda wa utulivu kuwaambia.Elezea jinsi unavyojisikia uoga,furaha au hofu na uwaulize kama wana ushauri wowote kwako.hiki kitawasukuma wao kukusaidia na kujua kua sasa hivi umekomaa na unakua mtu mzima.

Kumbuka.kuona siku zako za mwezi ni kitu cha kawaida katika maisha na wasichana wote watapata siku zao hivi karibuni au badae,usijaribu kusumbuka na hili jambo mwenyewe.Kwa kuliongelea unatengeneza njia madhubuti za kupata msaada.

Share your feedback