Una afya bora kwa kiasi gani?

Fahamu ni ipi kati ya tabia zako zinakufaa...

Tabia kama vile kula mboga freshi na kufanya mazoezi ni nzuri kwa mwili wako: tabia kama vile kula peremende na vyakula vilivyokaangwa, kuvuta sigara na kunywa pombe kupita kiasi ni mbaya. Inachukua kwa wastani wa wiki tatu kuwa na tabia, kwa hivyo nenda nje na uanze kuwa na tabia nzuri – utahisi mwenye furaha, mwenye ujasiri zaidi, thabiti na mwenye afya.

Fanya jaribio ili kujua jinsi:

Maagizo Soma maswali hapa chini. Chagua jibu A, B au C la kila swali kisha ubofye kwenye ukurasa unaofuata ili kuona jinsi ulivyo na afya.

  1. Kula kitafunio kati ya milo si vibaya sana mradi tu usawazishe vizuri!

Je, wewe: A: Kitafunio kwenye aina zote za vyakula, hata tunda? B: Kula kitafunio hata kama huhisi njaa? C: Kitafunio kwa chokoleti, keki, peremende, chakula kilichokaangwa kama vibanzi/chipsi?

  1. Ni muhimu sana kufanya mazoezi au aina fulani ya shughuli ya furaha inayofanya mwili wako kuchezacheza.

Je, wewe: A: Huenda nje na kutembea kila siku, hata kama ni kucheza mchezo wa furaha, kukimbia au kutembea nje na marafiki? B: Hucheza tu spoti au kufanya mazoezi yakiwa sehemu ya darasa au yaliyoandaliwa shuleni. C: Hupendelea kusalia ndani ya nyumba na kutowahi kuenda nje sana?

  1. Ni nini kinachofanyika wakati mtu aliye karibu nawe anapovuta sigara?

Je, wewe: A: Humwambia jinsi ilivyo vibaya kwake na kwako? B: Huipuuza? C: Humuliza ikiwa anaweza kukupa sigara yoyote?

  1. Ni wikendi, wakati wa kununua chakula kilicho tayari kuliwa! Machaguo ya mlo wako ni wali na saladi au vibanzi.

Je, wewe:
A: Huchagua wali na saladi. B: Hula vyote vitatu. C: Hula vibanzi tu.

  1. Ukiwa na kiu, unapenda kinywaji gani?

A: Glasi kubwa ya maji B: Wakati mwingine maji lakini ninapendelea vinywaji vitamu! C: Nitakunywa chochote lakini si maji!

Share your feedback