Marafiki zangu wa Mtandaoni

Jinsi ya kuwa salama

Mawazo yako (19)

Mambo, jina langu naitwa Asha, naishi na mama na dada yangu hapa Mwanza. Kwa sasa sijafanikiwa bado kupata smatfoni ila huwa huwa namuomba dadangu simu yake angalau niweze kuingia kwenye mitandao ya kijamii.

Nimekuwa nikitumia mtandao wa facebook kwa kipindi cha miezi minne sasa. Nina marafiki wengi na wengi wao ni watu ambao sijawahi hata kuonana nao. Kuna kaka mmoja ambaye nimekuwa nikichati nae kwa muda sasa na ameniomba tukutane. Mara zote amekuwa akiniambia kwamba mimi ni mrembo na kwamba tunaendana sana kama tutakuwa wapenzi.

Kiukweli nilikuwa naogopa sana kumwambia dada yangu na hata marafiki zangu kwani nilihofia wangenihukumu kwa kitendo hicho ama wangeniambia huku ni kuhatarisha maisha yangu. Lakini moyoni niliwaza kwamba yawezekana hii ilikuwa ndio fursa yenyewe ya kukutana na mtu ambaye angeweza kuja kuwa mume wangu. Kwa kweli nilitamani sana kukutana nae. Lakini nilikuwa sielewi nifanye nini.

Lakini wakati ambapo moyo wangu ulipokuwa ukiniambia, huyu anaweza kuwa ndiye mtu anaenifaa! Kulikuwa na sauti nyingine inaniambia " unatakiwa kuwa makini" Sikujua cha kufanya hivyo nikapata ujasiri wa kumweleza dada yangu kuhusu hilo.

Mmh haikuwa rahisi kwakweli, lakini nafurahi kwamba niliweza kuongea nae. Kwa sababu ushauri alionipa ulikuwa na msaada mkubwa mno, na hata alinisisitiza kwamba kila nitakapokuwa nahitaji msaada nisisite kumwambia

Huu hapa ndo ushauri alionipa.

Alisema "Asha, huwa inaweza kuwa jambo gumu sana pale unapoanza kujenga hisia na mtu fulani, tena kama ndo umekutana nae mitandaoni. Lakini tunatakiwa kuwa makini sana kwani wakati mwingine inaweza kukuweka hatarini.

Ni rahisi mno kwa watu kuigiza ama kujifanya kuwa na sifa fulani katika mitandao wakati kiuhalisia hawapo hivyo. Alinipa mfano akasema " Unajua hatujui kama picha ambazo watu huziweka katika mitandao ya kijamii ni zao kweli. Huyo kijana unayedhani unampenda unaweza ukakuta hata ni mtu mzima, ambaye anatumia mtandao ili kurubuni wasichana.

Wakati mwingine tunaweza kujisikia huru na virahisi kabisa kuwambia watu siri zetu kwenye mitandao ya kijamii kuliko tuwapo ana kwa ana. Lakini hili huweza kutuweka hatarini na hata watu kuweza kutudanganya. Kama mtu ataniahidi kunipa kitu kupitia katika mitandao au hata kunisifia sana, huwa moyoni nasema kwamba lazima kuna kitu atakuwa anakitaka kwangu.

Hivyo sote tunatakiwa kuwa makini sana tunapokuwa tunachati na watu mitandaoni na hasa pale watakapohitaji kuonana na sisi ana kwa ana.

Ila kama basi utaamua kwenda kuonana na huyo mtu hakikisha unakwenda na rafiki yako lakini pia kumbuka kuwajulisha watu wengine mahali unapokwenda. Kamwe usiende peke yako.Pia Kutana nae mahali ambapo sio mafichoni na iwe mchana na pawe na watu wengi ambao wanaweza kukusaidia pale utakapohitaji msaada.

Na Kamwe usipande nae mtu huyo usiemfahamu kwenye gari binafsi au hata kwenye basi.Na usimueleze mahali unapoishi.

Mwishoni niliamua kutokwenda kukutana nae na sijawahi kujutia uamuzi wangu huo. Ushauri niliopewa na dada yangu ulinisaidia mno, hivyo kama utajikuta kwenye mazingira kama yangu hakikisha unazungumza na mtu unayemuamini.

Je Dondoo za Sista zimekuwa za manufaa kwako? Basi tupia maoni yako hapo chini.

Share your feedback

Mawazo yako

Vzur sana sster yanatokea sana.matatzo kuptiq mitqndqo

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Mambo best

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Endelea kuwa. Na msimamo

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Ndio zinafaida

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Vizuli

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Zimenisaidia Sana, Asante!

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

nzur sana

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Et e

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Safi sana sister ana maamuzi na ushauri mzuri kama usingemsikiliza dunia ingekufunza nawe nakutakia hongera kwa usikivu wa dadaako!

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Safi sana sister ana maamuzi na ushauri mzuri kama usingemsikiliza dunia ingekufunza nawe nakutakia hongera kwa usikivu wa dadaako!

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Latest Reply

Vizur sana ana

safi

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

nimekuelewa ndugu

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Nimemuelewa ,,bila shaka tunatakiwa kuwa makin🙏

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Dah Kiukwel Zmekua na manufaa tena makubwa mno

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Mambo?

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Latest Reply

manbo?

kwema

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

ushauri mzuri sana

Machi 20, 2022, 8:25 p.m