Nilikuwa msichana maarufu

Lakini sikuwa mzuri

Marafiki ni muhimu sana. Ni watu watakaokusikiliza na kuhifadhi siri zako. Lakini kujua namna ya kuwa rafiki mzuri kwa kawaida si rahisi. Hiki ni kisa cha msichana mmoja.

Jina langu ni Lina. Nina miaka 15 na ninaishi Afrika Kusini. Nimekuwa na marafiki wengi lakini ninapoangalia nyuma sio wote waliokuwa wazuri kwangu. Wakati wangu mwingi wa kusoma nilikuwa nimezingirwa na wasichana wengi sana. Hawakujali kuhusu yeyote ila wao wenyewe. Hawakunitafuta na wangenihimiza kufanya mambo mabaya. Walicheka nilipokuwa jeuri kwa wazazi wangu. Walidhani kuwa hilo lilikuwa jambo zuri.

Sikutaka kuwapoteza kama marafiki kwa hiyoa nilidhania kuwa lilikuwa jambo zuri pia.

Tulikuwa wasichana 'wazuri' shuleni – maarufu sana wakati wote. Sote tulipata alama nzuri na tuliwacheka wasichana waliojitahidi darasani. Tuliwacheka na kuwaita wajinga.

Kisha siku moja wazazi wangu wakaniambia kuwa tulitakiwa kuhama mjini. Nilihuzunika sana. Niliwakosa marafiki zangu hata kabla ya kuondoka. Sikujua ambacho ningeweza kufanya bila genge langu.

Nilijiunga na shule mpya. Ilikuwa na wanafunzi wengi ambao sikuwajua. Sasa sikua mtoto mzuri tena. Nilikuwa mtoto mgeni. Ni mimi niliyekuwa peke yangu.

Nililia siku hiyo ya kwanza. Nililia kwa muda mrefu shulen.

Lakini baadaye nikakutana na Marvi. Alikuwa imara. Alijua tofauti kati ya baya na zuri na alitetea kilichokuwa kizuri. Alinipokea vizuri na kunifanya kujisikia kukaribishwa. Tumekuwa marafiki wazuri tangu siku ya kwanza nilipokutana naye. Nimejifunza mengi kuhusu rafiki wa kweli akiwa upande wangu.

Amenifundisha kuwa urafiki unahusu kushiriki mawazo na hisia zako. Pia unahusu kushiriki safari yako kupitia matukio ya maishani – mazuri na mabaya.

Pia alinionyesha kuwa urafiki unahusu kuwa mtu mzuri wala si kuwadhuru watu walio karibu nawe au kutowajali. Sasa nimegundua kuwa sikuwa rafiki mzuri mwanzoni.

Nimejifunza mengi kuhusu kuwa rafiki. Siwacheki wasichana wengine tena au kutoa maoni mabaya. Sisengenyi watu wengine. Mimi ni mzuri kwao, na wananisaidia.

Rafiki mzuri ni dada wa kweli na baraka maishani mwako.

Share your feedback