Barua ya mapenzi kwangu

Kwa sababu wewe ni wa thamani!

Wasichana wengi wanasumbuka kuwa wajasiri na kujiamini. Hivi ndivyo Oneli (14) na Kaneno (14) walivyojifunza kujipenda. Hizi ni barua za mapenzi walizojiandikia.

Mpendwa Oneli,

Umetoka mbali kuanzia siku ulizofikiria ulikuwa na sura mbaya na mjinga. Sasa umegundua kwamba wewe ni kama kila msichana duniani, wewe ni wa pekee na kwamba kufurahia jinsi ulivyo hukufanya uwe mtu mzuri ndani na nje. Umekubali kwamba unapenda kuwa mndani na unapendelea kuchukua muda wako Jumamosi usiku ukifanya kazi zako za nyumbani badala ya kwenda kwenye starehe. Ijapokuwa wewe una haya, umejifunza kujizungumzia na kusikilizwa.

Huruhusu kamwe ikuzuie kusikilizwa, kama wakati ulipojipa changamoto ya kuanza kuinua mkono wako darasani wakati unajua jibu sahihi au ikiwa kuna kitu ambacho huelewi.

Una ujasiri na una ndoto kubwa, kama kutaka kuanzisha shirika ambalo linawasaidia wasichana kuwa jasiri na wanaojiamini. Hii itatusaidia sisi wasichana kukabiliana na ulimwengu kwa ujasiri na kwa ushupavu.

Mpendwa Kanelo,

Daima umekuwa mtu mwenye ujasiri. Hujawahi kujidharau au kuzingatia yale wanayosema watu juu yako. Ninajivunia kwa kufanya kazi kwa bidii na kufanya ndoto zako zitimie. Baada ya siku kadhaa usome kwa bidii, sasa wewe ni mwanafunzi wa uigizaji katika Shule ya Kitaifa ya Sanaa. Umekaribia kuwa mwigizaji wa kike. Ukiendelea kufanya kazi kwa bidii, kufanya kazi zako zote za shule, kufanya mazoezi na kuzingatia masomo yako, ulimwengu utajua kuhusu wewe. Endelea kujituma. Wakati wako utafika.

Je, kwa nini usijiunge na mamilioni ya wasichana ambao wanaweka msimamo wa kujipenda na ujiandikie barua? Unaweza!

Share your feedback