Ota ndoto kubwa. Mustakabali ni wetu!
Hamjambo Wanadada!
Jina langu ni Chikondi na natoka Zambia. Mwezi uliopita shuleni, mwalimu wetu wa kuigiza alitusimulia hadithi ya ajabu kuhusu mwanamke anayeitwa Oprah Winfrey. Alilelewa na mama mmoja wa huko Mississippi, Marekani. Utotoni mwake, aliweza kuishi maisha magumu ya umaskini na ubaguzi wa rangi. Lakini hakuruhusu mambo haya kusitisha kutimiza ndoto zake. Alipanda ngazi katika TV na Filamu na kuwa mwanamke wa kwanza mweusi kupokea tuzo la kipekee Hollywood. Hiyo inatia moyo sana!
Baada ya kusikia hadithi hii nilitafuta kwenye YouTube “speech Oprah Winfrey made” baada ya kushinda tuzo hio. Ilikuwa nzuri sana. Jambo alilosema na lililonipendeza sana ni:
"Nimewahoji watu waliopona baadhi ya mambo mabaya zaidi katika maisha yao, lakini jambo moja kuu ambalo wote walishiriki pamoja ni uwezo wa kudumisha matumaini ya siku nyingine nzuri, hata wakati wa siku zetu zenye giza zaidi. Kwa hiyo ninawataka wasichana hapa, sasa, kujua kwamba siku nyingine inawadia !"
Wasichana, Oprah Winfrey yuko sahihi kabisa! Siku nyingine imekaribia kwa ajili yetu. Sasa hivi, sisi wasichana duniani kote tuna nguvu zaidi ya wakati wowote ule, tuna uwezo zaidi wa kupata maelezo na tumeshirikiana zaidi kuliko awali. Sasa ni wakati wa kujiamini hasa katika ndoto zetu kwa sababu MUSTAKABALI NI WETU! Usije amini kwamba wewe ni mdogo sana au haufai kuwezesha ndoto zako zitimie .
Hotuba ya Oprah Winfrey kwa hakika hunifanya niamke na nikifikiria kuhusu jinsi mimi nilivyo pia na nguvu ya kutimiza ndoto zangu. Niliongea na wasichana wengine katika darasa langu na kwa pamoja tulipata wazo la kuendesha klabu ya uigizaji , baada ya kuhitimu shuleni, kwa wasichana katika jamii yetu. Kwa njia hiyo wasichana ambao hawakwenda shule wangeweza kujiunga pia. Wiki iliyopita tulionyesha mchezo wetu wa kwanza wa kuigiza kuhusu Malkia Amina wa Afrika.
Ninamshukuru Oprah Winfrey kwa msukumo wake, lakini pia ninajivunia sana kwa kuchukua hatua ya kuwasaidia wasichana katika jamii yangu. Kama naweza kufanya, nawe pia unaweza, unachopaswa kufanya ni:
Huwa unafanya nini unapopatwa na changamoto, je unaendelea kupambana tu kwa kile unachokiamini? wasaidie wasichana wenzako kwa kuwatia moyo ,tuandikie kwenye sehemu ya maoni hapo chini.
Share your feedback