Nilitengeneza tovuti kwa wafanyabiashara katika kijiji changu
Jina langu ni Kechi na natoka katika kijiji kidogo cha wavuvi kaskazini mwa Nigeria. Nilipokuwa nakua, nilidhani hakuna lolote la kufanya katika kijiji changu. Daima nilikuwa na ndoto ya kutorokea mahali kwingine. Mahali ambapo kuna nafasi zaidi kwangu... Mahali ambapo ningeweza kuwa na maisha bora na kuleta tofauti.
Siku moja, shirika la ufadhili linalolenga kuwasaidia wasichana kujifunza ujuzi mpya liliendesha shindano katika eneo langu. Mshindi alikuwa asajiliwe katika kozi ya taaluma ili kujifunza kuhusu tovuti na usimbaji kwa njia fiche. Hiyo ni nzuri!? Nilidhani kutoenda shule kutanizuia lakini hakukuwa hivyo. Kozi za taaluma hukufunza kila kitu kuanzia mwanzo. Lazima nishinde shindano hili!
Changamoto ilikuwa kupata wazo la kusaidia kuimarisha jamii. Wazo bunifu zaidi lingeshinda! Kwa muda nilihisi nimekwama kwa sababu nilifikiria hakukuwa na matumaini katika kijiji changu lakini changamoto hiyo ilibadilisha mawazo yangu na jinsi nilivyoona mambo. Nilitoka na nikaanza kuzungumza na watu kuhusu matatizo yao. Nilimuomba mama yangu anisindikize ili niwe salama zaidi kwa kuwa nitakuwa nikiongea na watu ambao siwajui.
Baada ya mahojiano yangu yote nikaanza kugundua tatizo moja. Kulikuwa na vipawa vingi katika kijiji changu lakini watu nchini Nigeria hawakujua. Tuna mazao mengi, kuanzia vyakula , mavazi, hadi vikapu vya mbao, lakini hakukuwa na yeyote wa kuvinunua. Aha! Kama ningeweza kuunda tovuti ya wafanyabiashara ingewapa jukwaa la kuuza bidhaa zao na hiyo inaweza kuleta pesa katika kijiji chetu. Niliwasilisha wazo langu kwa shirika hilo la ufadhili na nikashinda! Nilifurahia sana na kujivunia hilo.
Ni ajabu kwamba sikuhitaji kutoroka kwenda mahali pengine. Ningeweza kutimiza ndoto zangu mahali nilipokuwa. Wakati mwingine unahitaji kutoka nyumbani kutimiza ndoto zako, lakini kama huwezi, usidharau nafasi zote ulizonazo mahali ulipo!
Pia, usidharau uwezo wa ndoto yako. Nilidhania nilikuwa natengeneza tovuti kwa wafanyabiashara tu bali ilikiwa kitu kikubwa zaidi. Baada ya kozi ya taaluma nilianza pia kuwafundisha wasichana wengine kuhusu tovuti na usimbaji kwa njia fiche. Pesa za ziada kutoka kwa wafanyabiashara zilitumika kujenga hospitali mpya ya kijiji. Mambo haya yote mazuri, kutoka tu kwa msichana mmoja mwenye ndoto.
Kwa hiyo, Mwanadada, jiamini, amini ndoto zako na kila kitu kinawezekana!
Kwa hiyo mnaonaje wasichana, je ungependa kusoma kozi fulani ya kiufundi? Ni vitu gani hasa ungependa kujifunza,tungependa sana kusikia stori yako- Jiamini, amini ndoto zako na kila kitu kinawezekana..
Share your feedback