Jinsi nilivyopata nguvu baada ya wazazi wangu kufariki.
Mambo Vipi Wasichana!
Nataka kuwasimulia stori yangu...
Maisha yalikuwa mazuri, kila kitu kilikuwa kilikuwa kinaenda vizuri mpaka pale tulipopatwa na hili janga. Nyumba yetu iliteketea kwa moto na niliwapoteza wazazi wangu wote. Kilikuwa kipindi cha huzuni sana kwangu kwasababu ni mwaka tu ulikuwa umepita tangu bibi yangu kipenzi afariki. Kwa hiyo hili tena ndo ghafla nikawa yatima. Nilijisikia uchungu na hasira sana na kitu cha haraka nilichowaza kichwani ni kwanini haya yananipata ?
Katika hiki kipindi sikuwa na nguvu ya kusimama tena. Kitu kipekee kilichokuwa kinazunguka kichwani ni "kwanini mimi, kwanini mimi, kwanini mimi?" Kadri nilivyokuwa naendelea kujiuliza "kwanini mimi?" ndivyo nilivyo jisikia vibaya zaidi. Huo msongo wa mawazo ulifanya mambo kuwa magumu zaidi.
Ila ghafla wazo fulani liliniijia kichwani . Nikaanza kukumbuka, Nilipofiwa na bibi yangu nilikuwa nilijawa na huzuni sana lakini baada ya muda nilianza kujisikia poa tena, marafiki zangu nao walikuwa ni msaada mno. Nikasema kama niliweza kukabiliana na Ile hali basi hata hili nalo nitalimudu pia. AU SIO? NDIYO, Hii ni kweli kabisa. Nilianza kupata nguvu na kujiamini kwa kuwaza mawazo chanya na kwa kuyasema kwa sauti. Nikajikuta nayakumbuka yale magumu yote niliyowahi kuyapitia, na zile nyakati nilizokuwa nikianguka nikaweza kusimama tena. nikajiambia tu Kwa hiyo sasa kwa nini sasa hivi nishindwe?
Kamwe huwezi kufahamu njinsi ulivyo imara mpaka pale ambapo kuwa jasiri ndio chaguo pekee ulilonalo. Baada ya mazishi nilikwenda kuishi na mjomba na shangazi yangu na kiukweli toka siku Ile wamekuwa msaada mkubwa sana kwangu . Walinisaidia kuelewa kwamba uchungu na hasira niliyokuwa ilikuwa kitu cha kawaida lakini ilipaswa kufika mahali ambapo natakiwa kuwa kusimama na kupambana. Na nilifanya hivyo.
Shangazi alinifundisha maneno niliyotakiwa kuyarudia rudia kuyasema ili niweze kujipa moyo. Kila siku nilijiambia "kama niliweza kufanya hivyo huko nyuma, hata sasa nitaweza.". Mimi ni jasiri Mimi ni mshindi Hakuna kitu kinachoweza kunizuia."
Miezi michache baadae baada ya kuyarudia rudia haya maneno, nilianza kujisikia vizuri na mwenye nguvu. Huu ndo mwanzo wa kusonga mbele kwenye safari yangu, unapaswa kujiamini na kuwa jasiri. Kwa hiyo sasa wakati mwingine utakapokuwa kwenye wakati mgumu au unajisikia huzuni sana, unatakiwa kufanya hivi:
Share your feedback