Mambo 4 ambayo huwezi kufundishwa shuleni

Kuwa bora Kadri unavyoweza

Tunajifunza mambo mengi sana ya muhimu shuleni, hesabu, sayansi, kusoma na kuandika na huo ni mwanzo tu! Lakini kuna vitu ambavyo hatujifunzi tukiwa shule, ni maisha pekee ndio yanayoweza kutufunza vitu hivyo. Je ni vitu gani hivyo?

#MALENGO

Huwa tunaviona vitu hivi kupitia mitandao ya kijamii, sio? #MALENGO! Lakini hatupaswi kulitumia neno hilo kumaanisha #malengoyakimapenzi au #kuwanaafyabora. Badala yake kila mmoja wetu anapaswa kuwa na malengo binafsi. Kama una ndoto za maisha yako ya baadae, pambana uzitimize.

Andika malengo unayotaka kuyatimiza ndani ya mwaka mmoja ujao. Je ni kwenda chuo kikuu? Kuanzisha biashara? Au kutafuta kazi? Hata kama yanaonekana kuwa malengo makubwa, usiogope. Vunja vunja malengo hayo ziwe hatua ndogo ndogo na kisha Anza na malengo yaliyo rahisi kuyatimiza.

Anza kuwa na bajeti

Moja ya kanuni kuu katika maisha ni, kamwe usitumie pesa nyingi kuliko kipato chako. Anza kutunza pesa, hata kama ni kiwango kidogo. Pale unapotaka kununua kitu, hakikisha unakifikiria kama kweli unakihitaji kitu hicho. Wakati mwingine matumizi mabovu ya fedha au manunuzi ya hovyo vinaweza kuwa kizuizi cha kutimiza ndoto zetu.

Tunza afya yako

Safari ya kutimiza ndoto zako sio kitu rahisi hivyo unapaswa kuwa na nguvu na afya ya kuzidi kusonga mbele. Ili mwili wako uwe na nguvu ya kufanya hili lazima uwe na afya njema. Mazoezi husidia kuimarisha afya ya akili. Hii inakupa nafasi ya kujenga kujiamini na kuwa na mawazo chanya ili kukusukuma kuzitimiza ndoto na kutokujisikia kukata tamaa.

Muda ni dhahabu

Hivi umewahi kusikia huu msemo? Inachomaanisha ni kwa muda ni kitu muhimu sana. Muda hupita haraka na kamwe huwezi kuurudisha nyuma. Hivyo tunatakiwa kuwa makini tunavyoutumia muda tunaopewa kwa kufanya vitu vilivyo vya na umuhimu kwetu.

Hivyo msichana, kuwa na ndoto na malengo, tunza pesa na anza kuyafanyia kazi. Utazisogelea ndoto zako katika muda sio mrefu.

Share your feedback