Fanya sehemu yako.

Pata uzoefu katika kazi unayoitaka

Mambo Vipi Wasichana,

Sisi sote tuna ndoto na matarajio ya kile tunachotaka kukitimiza katika maisha, lakini ni huwa rahisi kuingiwa na hofu ama kujisikia kuchanganyikiwa kuhusu wapi pa kuanzia . Usiogope… Hakuna haja ya kujiskia kuogopa! Kitu cha msingi ni kuanza kidogo kidogo.

Hatua kubwa ya kwanza ni kujua kile unachokitaka.

Unapaswa kwenda katika ofisi mbalimbali na kujifunza vitu wanavyofanya. Hii itakusaidia kufahamu na kuamua unataka kuwa nani katika maisha yako,na ndio wakati wa kupima ndoto yako kama je ndio kazi unayoitaka kwenye maisha yako au la!

Kuanza: Tafuta kampuni au shirika linalofanya kazi katika sekta ambayo unavutiwa nayo. Omba nafasi idara ya uajiri, na waeleze kuwa unatafuta ajira ya kujitolea ili kupata uzoefu. Kwa kawaida, hii inaweza kuwa kwa siku moja au wiki nzima. Kanuni ya kwanza. Daima hakikisha ni mazingira salama. Omba mtu mzima akusaidie kutafuta shirika na kuhakikisha ni sahihi na kwamba hautokuwa hatarini.

Kuwa msaada: Hivi unajuwa ni watu gani hupendwa na watu? Watu ambao ni msaada kwa wengine.

Jitambulishe kwa watu wanaokuzunguka, waulize kuhusu wanachofanya, waambie kwanini uko tayari kushirikiana nao na toa msaada wakati wowote unapohitajika. Watu huwa wanashukuru pale tunapokuwa na bidii katika kazi.

Uliza tu: Huwa hakuna swali la kijinga! hata siku moja, Mojawapo ya faida ya ajira ya kujitolea kukuza uzoefu wako ni kwamba, unapata kukutana na watu ambao wana majibu ya maswali yako, na huenda wakakupa taarifa nyingine muhimu ambazo hukufahamu kama unazihitaji.

Fanya sehemu yako: Jifanye kama mtaalamu. Kumbuka kuwa kila fursa tunayopata kuelekea kwenye ndoto zetu ni ya muhimu. Kwa hivo tumia kikamilifu nafasi unazozipata. Fika mapema kazini, usiongee na simu yako uwapo katika mkutano au wakati wa kazi.

Kujaribu haya madogo kunakupa ujasiri zaidi wa kusonga mbele ili kutimiza ndoto zako.

Kila la kheri Msichana, kuwa na ujasiri na usiache kujiamini .

Share your feedback