Nitawezaje kupata kazi?
Rafiki yangu kipenzi Mwantumu huwa yupo bize sana kila wikiendi akiuza katika genge lao la matunda. Kaka yangu huwa anarudi usiku sana kutoka kazini kila siku. Lina nae humsaidia kazi mama yake kwenye saluni yake, hufanya kazi kama zile za kufagia nywele na hata wakati mwingine huruhusiwa kusaidia kuosha nywele za wateja.
Nilituma maombi ya kazi katika migahawa yote iliyopo mtaani kwetu na maduka mbalimbali, lakini sikuweza kupata kazi. Sikuweza kufanikiwa kupata nilichokitafuta sababu sikuwa na uzoefu wa kutosha.
Ninapenda mavazi, lakini wasichana wote wanaofanya kazi katika maduka ya nguo wanaonekana wakubwa kidogo kwangu na ni kama wana uzoefu wa kuuza. Hivyo isingekuwa rahisi mtu yeyote kunipa kazi.
Kwa kuwa marafiki zangu walikuwa wamebanwa na kazi, niliamua kufanya jambo la maana. Nilisoma jinsi ya kukata na kushona nguo. Niliazima vitabu kutoka kwenye maktaba na kuchunguza vitu kutoka mtandaoni, ukiongeza na ujuzi wangu nilioupata shuleni. Kwa njia hii, itanisaidia kuwa na uzoefu zaidi ifikapo likizo ijayo, naamini naweza kupata kazi.
Kwa kutumia fedha zangu za mfukoni, nilienda madukani kununua vitambaa vya kujifunzia kushona. Nilishona baadhi ya vitu vyangu vya kuendea shule. Watu wengi walinipongeza na kuniuliza ‘umepata wapi hiyo sketi yako?’’ na wengine walisema ‘’mkoba wako ni mzuri sana’’ “Ninapenda viatu vyako!”
Wikiendi iliyofuata nilienda kwenye soko lililopo mtaani kwetu na kuwauliza baadhi ya wamiliki wa maduka jinsi walivyoweza kufanya biashara na bei gani ningehitaji kuuza bidhaa zangu ili kupata faida. Nilimuomba mama anisaidie kulipa kodi ya chumba cha biashara, lakini nilimuahiidi nitamlipa ntakapopata pesa kutoka katika biashara yangu. Baada ya muda mfupi nilikuwa na uwezo wa kujilipia kodi kila mwezi bila kuomba msaada kwa mama.
Mwanzoni, nilipata tabu hasa pale ambapo watu wengi hawakutaka kunisaidia lakini badala ya kukaa tu na kusubiri kupata ajira niliamua kufanya kitu nilichokipenda na kilinipa faida.
Vipi wewe, je una kitu kinachosadia kukuingizia pesa? tungependa kufahamu zaidi ,tuelezee hapo kwenye sehemu ya maoni.
Share your feedback