Je unataka kuwa kama nani?

Mtu anayekuvutia ni bora kiasi gani? Hebu ngoja tuone

Maisha yanatatiza Sana. Tukiwa tumezungukwa na hamasa na mawazo ya watu wengi, kutoka kwa marafiki, ndugu, walimu, na wazazi, bila kusahau mtandao ya kijamii, wakati mwingine inakuwa vigumu Sana kujua nani umsikilize na maamuzi yapi ni sahihi au sio sahihi.

Sote tunao watu tunaowatazama kama mfano kwetu. Labda kwako wewe anaweza kuwa msichana fulani aishiye mtaani kwenu ambaye amefanikiwa kuendesha biashara yake tokea nyumbani, au anaweza akawa mwalimu ambaye ametambua uwezo wako na anakusukuma kufanya mambo makubwa zaidi, lakini pia anaweza akawa mjomba wako au shangazi ambao wamejawa na hekima na huwa wanakutia moyo au ni binti fulani huko Instagram ambaye anakuvutia na kukuhamaisha kufanya mambo makubwa. Je hivi Hawa watu tunaovutiwa nao wanaweza wakawa washauri wazuri kweli?

Je ni jinsi gani unaweza kumtambua na kumuamini mtu ili aweze kukupatia ushauri na muongozo wa namna ya kufanya maamuzi sahihi?

Hebu anza na hatua hizi rahisi.

1. Tengeneza orodha

Andika vitu unavyovithamini katika maisha yako, kitu gani kinakusukuma kutaka mshauri na nini hasa unakiihitaji kutoka kwa mshauri huyo. Hii itakusaidia kupata picha ya kitu gani hasa unakiihitaji.

2. Anzisha mazungumzo

Kama utajisikia huru kuanzisha mazungumzo na watu unaowaona kama mfano wa kuigwa. Hebu waulize wanadhani mshauri bora anatakiwa kuwa na sifa zipi na je wanadhani wao ni wanaweza kuwa washauri wazuri, na je wanafikiri Kuna umuhimu wa kuwa na mshauri? Andika maoni ya kila mmoja wapo Kisha linganisha maoni ya yupi unakubaliana nayo zaidi. Mawazo ya kila mmoja wao yatakusaidia kujua yupi hasa atakufaa kama mshauri. Inawezekana wote kutokuwa na vigezo lakini wanaweza kupendekeza mtu atakaye kufaa. Sasa, utaanzaje kuwauliza haya maswali ?

3. Chukua hatua

Kama ni mmoja Kati ya watu unaowafahamu waombe japo dakika 5 tu za kuzungumza nao. Halafu kuwa muwazi- waambie ukweli kwamba ungependa sana kama utapata muongozo na msaada kuhusu maisha yako, na waeleze je watakuwa tayari uwamini na wataweza kukufichia siri zako na wakati huo huo wanakushauri bila kukuhukumu? Kwa asilimia zaidi ya tisini na tisa watafurahi na watakuwa tayari kukusaidia. Ikiwa rafiki yako amempendekeza mtu fulani ili akusaidie, muombe rafiki yako akutambulishe kwa mtu huyo, iwe ni kwa barua, simu au hata Ana kwa Ana. Kumbuka, unapokwenda kuonana na mtu hakikisha unaenda na mtu atakayekusindikiza lakini pia hakikisha umetoa taarifa kwa mtu mzima na mueleze unapokwenda, na pia simu yako hakikisha ina vocha ili ikitokea tatizo uweze kupiga simu haraka.

Je huoni kama imekaa poa sana kuwa na uwezo wa kupata washauri wengi wazuri? Mshauri sahihi yupo sehemu katulia anakusubiri wewe hapo.

Share your feedback