Furahia na uwe mbunifu na malengo yako
Kila mtu ana mipango ya maisha ya baadae. Mbinu bora ya kufanya mipango yako itimie ni kuwa na ubao wa ndoto zako. Hii inakusaidia uone matokeo ya ndoto zako na kuzifanya ziwe za ukweli na zinazoweza kutimia.
Kabla ya kuanza, ni muhimu kuwa na malengo thabiti. Ubao wa ndoto zako lazima uwe na picha za unachotaka kuwa, unachotaka kutimiza, maisha unayotaka kuishi na unavyotaka kuwa katika siku za baadaye.umeelewa? Sawa, sasa tuanze!
Unachohitaji kufanya:
Chukua karatasi ngumu (kama manila hivi).
Mkasi na gundi.
Chukua majarida au magazeti ya zamani.
Angalia katika majarida na uchague picha zinazofanana na taswira ya maisha bora unayotaka kuyaishi katika siku za baadaye. Hizi zinaweza kuwa picha za watu wanaokuhamasisha, maeneo ambayo ungependa kutembelea, mambo unayofurahia kufanya, kazi yako unayotamani. Huu ubao wa ndoto zako ni wako binafsi kwa hiyo hakuna picha iliyo sahihi ama isiyo sahihi. Waza mambo makubwa ya kuthubutu iwezekanavyo.
Kata picha zinazokuhamasisha na uzibandike kwenye karatasi ngumu uliyonao.
Tafuta au andika nukuu za kutia motisha na uzibandike kwenye ramani ya ndoto zako.
Bandika huu ubao wa ndoto zako mahali panapoonekana, mahali ambapo utaweza kuiona kila siku na kuyakumbuka malengo yako unaweza kuiweka katika ukuta wa chumbani au katika mlango.
Vipi inaonekana ni rahisi na ya kufurahisha eh? Ni wakati wako kujaribu.
Sote tunazo ndoto za siku zijazo lakini kamwe haziwezi kujitimiza zenyewe. Tunapaswa kuzifanyia kazi na kujishughulisha haswaa. Ubao wa ndoto zako utakusaidia kubaki na mawazo chanya kuhusu kesho yako na itakufanya usikate tamaa pale mambo yanapokuwa magumu.
Share your feedback