Vidokezo hivi vinaweza kusaidia!
Vipi dada! Fikiria kuhusu hili – Unapopanda mbegu katika udongo haiwezi kumea kwa siku moja. Kulingana na kile ulichokipanda inaweza kuchukua wiki, miezi au hata miaka kabla ya kuona kitu chochote! Na hata wakati umepanda kitu chochote huwezi kukipanda tu na kukiacha na kuondoka. Lazima ufanye kazi, kumwagilizia mbegu maji ili kuhakikisha udongo una virutubisho vya kutosha ili kumea.
Je! Si hii inalingana na ndoto zetu? Ndoto zako ni kama mbegu, lakini badala ya kuzipanda ardhini zimepandwa ndani yako. Sote tuna mbegu za ukuu ndani yetu. Bila kujali wewe ni nani au umetoka wapi kuna ukuu ndani yako.
Unaweza kuwa unawaza – Ninazo ndoto nyingi lakini ni lini zitatimia?
Kama mbegu udongoni, kuna kipindi cha kusubiri kati ya wakati unapoamua kufuata ndoto zako na wakati unapoanza kuona maendeleo fulani. Kipindi hicho cha kusubiri kinawezakuwa cha kuchanganya, lakini hapa kuna hatua kadhaa za kukusaidia kufaulu.
1. Kumbatia safari
Kumbuka kwamba maisha ni safari ndefu sio mbio fupi. Ukuu hautafanyika kwa siku moja na wala ndoto zako pia. Mambo mazuri huchukua muda, hivyo kuwa na subirá kwa ajili ya ukuaji wako. Maendeleo ya muda mrefu BADO ni maendeleo.
2. Furahia safari
Unapotumia muda mwingi ukiwaza mambo yote ya kushangaza unayotaka kufikia siku zijazo,maisha ya kila siku yanaweza kukosa ladha. Siri ya kuwa na furaha ni kutumia siku zako kufanya kile unachopenda.Hakikishaunapanga ratiba ya shughuli za kufurahisha kama vile kwenda matembezi na marafiki au kutafuta mapendeleo mapya.
3. Wakati wa safari Tafakari
Wakati mbegu yako inamea itapitia misimu tofauti. Kutakuwa najua lakini pia kutakuwa na siku za mvua. Kutakuwa na siku nzuri, na vilevile siku mbaya wakati unapohisi ni kana kwamba hufanyi maendeleo lakini hilo halifai kukuzuia kufuata ndoto zako. Kuchukua muda wa kupumzika na kutafakari kunaweza kukukumbusha safari uliyotokana kukupa motisha unaohitaji kusonga mbele.
Share your feedback