Jinsi ya kumtambua mshauri anayekufaa.
Upo katika umri ambao unayo maswali mengi kuhusu mambo mengi muhimu. Kuanzia maswala ya mahusiano mpaka yale yanayohusu maamuzi makubwa katika maisha, wakati mwingine huwa unatamani kama ungekuwa na mtu ambaye unaweza kumfuata ili akupe ushauri sahihi ambao utakusaidia unapofanya maamuzi.
Mshauri ni mtu unayeweza kuwasiliana naye na ambaye anaweza kukuelekeza na kukuwezesha ufikirie kwa kina, na kukufanya ufanye maamuzi yako mwenyewe kuhusu mambo fulani ila mwenye maamuzi ya mwisho utabakia kuwa wewe mwenyewe.
Unaweza kumtambua Mshauri anayekufaa kwa kufuata hatua hatua hizi tano rahisi.
Kama utaweza kuandika kile unachokihitaji hasa kutoka kwa mnasihi- ungependa akusaidie au kukupa mwongozo kwenye vitu gani hasa, je anapaswa kuwa mtu mwenye sifa/vigezo gani na ungependa kuwa na ukaribu nae kiasi gani, hii itakusaidia kupata picha hasa ya kile unachokitaka.
Andika majina ya watu wote ambao wanakusukuma kufanya kazi kwa bidii katika maisha yako, ambao wana hekima. Yawezekana akawa ni mjomba wako ambaye anamiliki biashara iliyofanikiwa, ama msichana fulani katika darasa la juu yako ambaye anakuvutia, au hata mfanyakazi fulani ambaye anafanya vizuri kazini kwake.
Pale utakapofahamu kitu gani hasa unakitaka kutoka kwa mshauri wako na kuorodhesha majina ya watu wanaokuhamasisha Sasa ni muda wa kuwafanyia utafiti. Mchunguze kila mmoja katika watu uliowaorodhesha. Je wana sifa Sawa na zako? Je wana muda na uwezo wa kukubali kuwa washauri wako?
Mpaka hapa naamini orodha yako itakuwa na majina machache tu yaliyobakia baada ya upembuzi. Anza kuongea na watu hawa, hasa kama ujasikia huru kufanya hivyo. Waeleze ndoto zako na malengo yako, na mwongozo gani hasa unauhitaji. Waulize maswali yote kuhusu vitu vinavyokutaziza shuleni, mazoezi ya nyumbani, kuhusu maisha yako ya baadae, na sikiliza majibu yao. Mara tu utakapofanya hivi utagundua yupi yupo tayari kukusaidia na nani hayupo tayari.
Ili kufanya uamuzi sahihi, hebu tafakari watu hawa walivyokufanya ujisikie, namna walivyojibu maswali yako na hata walivyokaa na kukusikiliza, na ndipo unaweza kufanya uamuzi. Pima faida na hasara kwa kila mmoja, na Mara utakapoamua Nani ungependa awe mshauri wako, vaa ujasiri na nenda kamwambie.
Kadri unavyofuata hatua hizi tano zitakazokusaidia kupata mshauri sahihi, haupaswi kupoteza matumaini. Mtu utakayemchagua kuwa mshauri wako lazima atajisikia vizuri mno kukupa msaada unaouhitaji.
Share your feedback