Pata Kazi Bomba!

Bado unaweza kufanikiwa hata kama hauna elimu ya chuo.

Je wajua watu wengi waliofanikiwa duniani hawakufanikiwa kupata elimu kubwa? Oprah Winfrey, ambaye ni mtangazaji maarufu kutoka amerika ambaye pia ni bilionea aliacha chuo na kujiunga na kazi japo alirejea masomoni baadae na kujipatia elimu yake ya chuo. Dunia imejaa watu wengi Sana kama yeye. Kama hautaki kwenda chuo au hauna nafasi ya kujiendeleza kimasomo, haimaanishi kwamba hauna uwezo wa kupata kazi unayoipenda.

Hizi ni baadhi ya mbinu unazoweza kuzifuata ili kufanya kazi ya ndoto yako kuwa kweli.

1. Kitu cha kwanza fikiria vitu ambavyo unavipenda orodhesha vitu unavyopenda kuvifanya, halafu chagua vitu bora, viwili. Na unaweza kujijengea uwezo kwenye vitu hivi kwa kujifunza kutoka kwa watu wengine, fanya utafiti, na anza kufanyia mazoezi. Labda unapenda uandishi- wasiliana na waandishi waliofanikiwa, waombe wakushike mkono na jambo la muhimu zaidi andika Mara nyingi kadri unavyoweza.

2. Fanya utafiti. Chunguza taaluma mbalimbali zinazofanana na vitu unavyovipenda. Unaweza kutumia mitandao au kwenda katika maktaba ama hata kuuliza watu. Unapokuwa karibu na mji, tembea na kijitabu cha kuandikia na andika baadhi ya biashara au vitu vinavyoendana vitu unavyovipenda.

3. Omba msaada ili kuandaa barua ya wasifu wako (CV) kisha anza kuzisambaza kwenye makampuni ama taasisi mbalimbali ambazo unatamani kuzifanyia kazi. Kumbuka kuandika barua ya maombi ukieleza kwanini unavutiwa kufanya kazi na kampuni husika. Unaweza kuomba kazi au kuomba nafasi ya kujitolea, au hata mafunzo. Vitu hivi mwanzo vinaweza visikupatie fedha lakini ujuzi utakaoupata utadumu muda mrefu sana.

4. Fanya kwa ajili yako kwani Nani amekwambia lazima ufanye kwa ajili ya mtu mwingine? Kama unakipaji au kitu ambacho watu wanaweza kukilipia, basi anza kukifanya Mara moja. Waandishi wa blogu, wacheza kikapu, waandika mashairi, madereva wa malori, dunia imejawa na watu waliofuata hobi zao, na vipaji vyao na kuzifanya kuwa biashara, hata wewe unaweza pia.

5. Usikatishwe tamaa fuata ndoto zako, hata iweje. Kama kazi yako inahitaji uwe na shahada, lakini hauna uwezo wa kwenda chuo hivi sasa, hii haimaanishi hautoweza kufanya kazi ya ndoto zako katika maisha yako ya baadae. Watu wengi huanza kufanya kazi kwanza ili waweze kujisomesha na wakati mwingine hupata msaada kutoka katika familia zao au serikalini.

Share your feedback