Tekeleza ndoto zako!

Fikiria kuhusu mambo makubwa

Tuna uhakika unachoshwa sana na kufikiria kuhusu unachokitaka ukitoka shule, au kazi ambayo unataka kuchagua. Ulipokuwa mdogo, ulikuwa na ndoto ya kuwa mjasiriamali, fundi wa nguo, mpishi, mwalimu, msaidizi dukani, mhandisi mitambo... na ndoto zote hizo kubwa zilionekana kuwa haziwezekani kabisa. Kwa kuwa sasa umekuwa mkubwa na mwenye busara, umegundua kwamba kufanikiwa katika kitu chochote maishani kunahitaji kazi nyingi ngumu na kujitoa. Na jambo muhimu ni hili... unaweza! Hakuna sababu ya kuwa nini usiweze kuwa kile unachotaka kuwa - ikiwa una ndoto lenga tu unachokitaka na ukitekeleze, hakuna chochote kisichowezekana!

Kwa hiyo, hivi ndivyo vinavyofanya ndoto zako kuwa mambo makubwa:

  1. Tafuta kinachokusukuma. Angalia watu katika jamii yako, na uandike kile kinachokusukuma. Inaweza kuwa mwalimu wako ambaye huchukua hatua ya ziada kuhakikisha kwamba unaelewa kazi yako; pengine ni mhudumu wa afya ya jamii ambaye sasa anaendesha kliniki yake mwenyewe; au mama mkubwa ambaye amekuwa akisimamia duka kubwa maisha yake yote.

  2. Uliza maswali. Ili mradi unahisi ni salama kufanya hivyo, anzisha mazungumzo na watu unaowaiga, waombe kama unaweza kuchukua dakika chache za muda wao na ujaribu kujua walivyoanza, wakikuelezea panda-shuka za safari yao na ushauri wanaoweza kukupatia. Utashangazwa jinsi utakavyohisi umepata motisha baada ya kusikia hadithi zao.

  3. Pata tajriba. Ikiwa umeamua njia ya mustakabali unayotaka kufuata, uliza kama unaweza kujitolea au uwafuatilie baadhi ya watu wako unaowaiga. Uliza kama unaweza kuomba kuwa mkufunzi au kufanya kazi bila malipo (usitarajie kulipwa lakini ukipokea kitu, ni bonasi!) Siku au wiki chache za kujifunza kutoka kwa watu wako unaowaiga kwa hakika kutakupatia mtazamo wa kile unachokipenda na usichokipenda.

  4. Weka malengo. Hadi sasa, huenda una wazo wazi la ndoto zako! Kwa hiyo ni wakati wa kuweka baadhi ya malengo. Andika malengo yako ya muda mfupi na malengo yako ya muda mrefu, kisha jipe muda wa kuyatimiza. Anza na malengo madogo na rahisi na kisha endelea kutimiza yale makubwa.

Kumbuka, hakuna kitu maishani kinachokuja kwa urahisi na hivyo kutakuwa na changamoto. Usiruhusu zikuzuie - unapojitahidi utatunukiwa!

Share your feedback