Hata sio mbinu ya siri kiivyo kwa wale wanaofahamu hili.
Mambo, naitwa Shanti na nina miaka 24. Inanifanya nijisikie mtu mzima. Lakini hili linamaanisha kuwa najua mambo kibao, yenye msaada. Mambo ya kiutu uzima. Na kutokana na mambo ninayoyajua yatakusaidia kupata kazi siku moja.
Kazi yangu hasa ni kufanya usahili wa watu pale wanaomba kazi katika kampuni yetu. Hii ina maanisha siku nzima huwa natakiwa kufanya maamuzi magumu kuhusu nani achaguliwe na nani asichaguliwe. Hakika yapo mambo KIBAO ya kukujuza, twende sasa.
Kitu Kikubwa cha Kwanza.
Unapoitwa kwenye usahili, hii humaanisha vitu vizuri viwili. Kitu cha kwanza humaanisha uliwasilisha wasifu wako (CV) safi kabisa, inaonyesha ulivyo makini na maisha yako. Jambo la pili, ina maana kuna mtu aliona wasifu wako na anahitaji kuzungumza na wewe. Mpaka hapa mambo yako safi kabisa.
Kabla ya Usahili.
Dah, usiwe hata na wasiwasi. Kama ukiwa na woga, itaonyesha kutokujiamini. Sababu hasa ya mtu kama mimi kuzungumza na wewe ni kwamba tunadhani unaweza kufanya kazi nzuri.
Nini nifanye ili nisiwe na wasiwasi, kuwa na ufahamu Zaidi wa vitu.
Tafuta taarifa kuhusu kampuni unayotaka kwenda kufanya kazi, na majukumu hasa ya kazi unayoitaka. Ingia kwenye tovuti na kusanya taarifa zote muhimu na unaweza kuuliza maswali. Hakuna kitu kinachofurahisha kama pale unapomhoji binti ambaye amejiandaa vizuri,
Pendeza Kulingana na Kazi Unayoiomba.
Kila kazi huwa ina vigezo vya namna gani unatakiwa kuvaa. Katika baadhi ya makampuni, utatakiwa kuvaa sare maalum kila siku. Na katika makampuni mengine, utakuwa na uhuru Zaidi wa kuvaa upendavyo. Kwa mfano dada yangu huvaa suruali ya jinzi kila siku anapokwenda kazini kwake. Kama nikivaa hivyo kazini kwangu yani lazima wataniletea shida.
Chagua vazi litakalokufanya ujisikie kuwa na ujasiri na kuonekana mwenye ufahamu wa kazi unayoiomba lakini Zaidi hasa likufanye ujisikie huru. Kuvaa mavazi ya mtaani yatakufanya uonekane huna adabu, lakini usipanie sanaa kuvaa . Kama haujui uvae nini, muulize mama yako, au hata shangazi, dada yako ama mtu yeyote ambaye unafikiri anaweza kukupa ushauri mzuri.
Kama huwa unapenda kujiremba, jirembe na kama hupendi poa tu, fanya unachopenda.
Msichana Mfanyabiashara Mwenye Kujiamini Na Mwenye Ushawishi.
Haya ndio umefika sasa hapa, inaweza ikawa katika ofisi au hata katika mgahawa. Labda kuna watu wengi halafu wapo bize na mambo yao. Upo sasa umekaa kwenye kiti koridoni,au mapokezi, hapa ndipo woga hukujaa sio?
Hata usiogope, hata kama unajisikia kujawa na wasiwasi hebu tafuta ule ujasiri uliopo ndani yako, ukiwa na wasiwasi unaonekana mtu bandia. Wanataka kumuajiri mtu halisi.
Na sasa ndio ule muda wa kuzungumza. Namna unavyosalimia kwa kushikana mikono ni jambo muhimu. Tabasamu ni muhimu. Watazame watu machoni. Dhibiti namna unavyopumua, ongea taratibu na kwa kujiamini. Kaa kwenye kiti ukiwa umenyooka vizuri, unatakiwa kuonyesha upo makini na kinachozungumzwa.
Mtu anayekufanyia usahili anapomaliza kukuuliza maswali na kutoa ufafanuzi, ni zamu yako sasa.
Je niulize nini? Unaweza kuuliza kitu chochote kinachohusiana na kazi. Kama ulifanya utafiti wako mapema naamini lazima utakuwa na maswali kadhaa, maswali hayakufanyi uonekane hauna adabu, yanaonyesha ni mtu mwelevu, yanakufanya usionekane kama mashine kwa kukubaliana na kila mtu.
Jambo Moja La Mwisho.
Kumbuka: Njia pekee ya kushindwa kitu ni kukikimbia. Kama utakutana na usahili mbaya, nimewahi kukutana nayo pia, kama mara sita hivi. Jifunze kutokana na makossa na jitahidi kufanya vizuri Zaidi mara nyingine.
Msichana hebu jipange sasa na ukafanye kitu.
Share your feedback