Njia nzuri za kuwa wa pekee na kukumbukwa
Tafuta mtu mwenye ufahamu - Weka sahihi
Tafuta mtu aliyefanikiwa - Weka sahihi
Tafuta mtu anayefanya kazi unayopenda - Weka sahihi
Tafuta mtu anayeweza kukusaidia kufikia malengo yako - Weka sahihi
Ikiwa umepata mtu ambaye amepata sahihi zote kwenye vikasha hivi basi hongera, umepata mshauri anayefaa! Kwa ujumla washauri ni watu wazuri ambao wako tayari kuwasaidia vijana kupata nafasi za kukua. Kuwatafuta ndio sehemu ya kwanza. Sehemu ya pili ni kuhakikisha una malengo wazi ya unachotaka kutimiza. Na sehemu ya tatu ni kuchukua hatua. Chukua hatua na uwasiliane nao kwa usaidizi, ushauri au motisha!
Unapowasiliana na mtu mtandaoni au katika maisha halisi, unapaswa kuzingatia kuwa mwenye kuvutia mara ya kwanza. Haya ndiyo unayoweza kufanya ili kuwa wa pekee:
FANYA UTAFITI WAKO- fahamu kadiri uwezavyo kuhusu washauri kabla ya kuanzisha mazungumzo. Hakikisha ni washauri wanaokufaa. Ongea nao kuhusu vivutio na hamu yao sio yako. Kuongea na watu kuhusu mambo wanayoyapenda huwachangamsha na huwafanya wawe wazi kukusaidia.
Wafanye wajihisi ni muhimu – kila mtu anapenda kusifiwa! Onyesha shukrani zako kwa wanavyofanya na uwafahamishe faida nzuri wanazo kwako. Kwa mfano, unaweza kuanza kwa kusema "Hujambo X, ninapenda sana unavyokuwa mkweli na mjuzi wa uongozi. Ilinihimiza kutumia sauti yangu kuwawezesha wasichana wengine. Ningependa kukuuliza maswali machache kuhusu maisha yako na nijifunze siri za ufanisi wako..."
Sikiliza kwa makini - Iwapo unakutana na mshauri ana kwa ana, hakikisha unaingia na TABASAMU nzuri sana na ufungue masikio ili usikie anachosema. Mhimize mtu huyo mwingine aongee kuhusiana na yeye unapokuwa ukisikiliza na kuchukua nukuu. Ushauri wao kuhusu jinsi ya kukua na kutimiza malengo yako ni wa thamani sana. Jaribu kuwa makini.
KUMBUKA Usalama kwanza!- Usikutane na wageni kivyako. Kimsingi, mshauri wako anapaswa kuwa mtu unayemjua tayari lakini wakati mwingine marafiki wanaweza kukuelezea kuhusu washauri wengine. Ikiwa unakutana na mshauri wako kwa mara ya kwanza, hakikisha ni hadharani. Kuwa na mtu mzima karibu na simu yenye muda wa kutosha wa maongezi ili uweze kupiga simu.
Kwa hiyo, kwa kumalizia, ujasiri ni muhimu! Usiogope au kujidharau. Fanya utafiti wako, waeleze kwa nini wanakuhimiza na uwasikilize wanapoongea. Kuwa mjasiri, dada, na uchukue hatua!
Share your feedback