Mjamzito mwenye matumaini

Kuwa na mtoto hakupaswi kukuzuia kusonga mbele.

Hakuna mtu anayeweza kubisha kwamba kuwa mjamzito ni jambo zito. Ni badiliko la maisha. Lakini haimaanishi umebadilika. Kuwa na mtoto inaweza kuwa mwanzo mpya kwako pia.

Mwanzo wa Mgumu
Angel hakutarajia kuwa mjamzito katika umri wa miaka 15. Mwanzoni alifikiria elimu yake imekwisha. Alihisi nafasi zake za kupata kazi nzuri na maisha mazuri zilikuwa ndio zimeyeyuka hivyo..

Usiku alikuwa hapati usingizi,mchana alikuwa akitembea huku akisinzia. Hakuweza kumwambia mtu yeyote kwa sababu hakuwa na ujasiri - lakini aliandika hisia zake zote katika kitabu chake cha kumbukumbu.

Kuwa muwazi
Haikuwa rahisi hadi pale ambapo rafiki yake kipenzi alipomshawishi sana kufunguka juu ya nini kinachomsibu ndipo mambo yalipoanza kubadilika. Shosti yake huyo alimtafuta nesi mmoja halafu akaweka miadi ya kukutana nae akiwa na Angel

Nesi hakumpima afya yake tu lakini alimshauri wapi anaweza kupata msaada.

Alipokuwa anaandika kwenye kijitabu chake cha kumbukumbu usiku huo, Angel alishangaa sana jinsi alivyojisikia vizuri baada ya yote hayo.

Hatua kwa hatua
Angel aliendelea, kutafuta msaada na taarifa zote anazozihitaji kadiri alivyoweza. Taratibu, huku akisoma kuhusu uzazi, au kwa kuwatazama kinamama wakicheza na watoto wao, alianza kupata matumaini ya maisha yake ya baadae.

Kurudisha shukrani
Usiku mmoja, alipokuwa akimalizia kuandika kwenye kijitabu chake akajikuta amefungua kurasa za nyuma, Angel akaamua kufanya jambo la ujasiri sana. Ndani ya moyo wake alijisikia kuwashukuru watu waliomsaidia wiki zilizopita, hivyo aliamua kushea nao stori yake.

Alikuwa anamini ikiwa kuna mtu ambaye anapitia mapito kama yake, basi ataweza kuwasaidia. kwa hiyo aliamua kutengeneza blogu na kuandika vipande vya stori yake humo.

Alishangaa kuona jinsi wasichana wengine walivyojitokeza fastaa kuchat naye huku wakisema kuwa walikuwa na mapito kama yake. Watu walimshukuru kwa kushea stori yake.Kwake yeye aliona amefanya tu msaada..

Kuwa na Matumaini Mapya
Angel alipopata mtoto wake, ilikuwa kazi ngumu, lakini kwa vile alikuwa anaelezea kwenye blogu yake hatua alizokuwa akipitia basi hakujihisi mpweke. Kila siku alijisikia vizuri kuwa mtoto wake alikuwa anakua vizuri.

Aliombwa hata kutembelea kundi la kinamama wa rika dogo kuzungumzia stori yake. Mwanzoni alikuwa anaogopa lakini baadaye akagundua kwamba ilikuwa kitu alichotaka kukifanya zaidi.

Alikuwa na wasiwasi kuhusu elimu yake kuwa asingeendelea, lakini Angel aligundua kwamba alikuwa bado anajifunza, kwa njia tofauti, na kuendeleza ujuzi mpya na ndoto mpya njiani zimejikeza.

Sote tuna vipaji ambavyo tunataka kuvikuza na vinaweza hata kuja kutulipa baadae, hebu tuelezee vipaji vyako kwenye sehemu ya maoni.

Share your feedback