Dondoo za Kufanya Wasifu(CV) Wako Kuwa Moto!

Je umepata kazi unayoitamani ? hatua ya kwanza ili kupata kazi ni kuwa na wasifu mzuri.

Ajira ni njia rahisi ya kukufanya kuwa na kipato na kutokuwa tegemezi. Ni jambo zuri mno kama wasifu wako utakuwa umechapwa kwa kompyuta, lakini usihofu kama hauna uwezo wa kuwa na kompyuta jirani, bado unaweza kuandika wasifu mzuri sana.

1. Orodhesha kazi zote ulizowahi kufanya.

Kama umewahi kufanya kazi inayofanana na unayoiomba hivi sana, iandike kuwa ya kwanza. Usihofu kama haujawahi kufanya kazi sehemu yeyote ile, fikiria sehemu ambayo umewahi kuwa na majukumu yoyote inaweza kuwa katika jamii inayokuzunguka, shuleni, inaweza ikawa ulikuwa kepteni wa timu au hata mwenye kujitolea. Lakini pia orodhesha historia ya elimu yako, mafanikio ( labda ulikuwa kiranja au ulipata cheti cha mwanafunzi bora) na usisahamu kuandika mawasiliano yako.

KIDOKEZO. Jaribu kuomba kazi ambazo zinaendana na kile ulichokisomea au ambavyo tayari unaweza kuvifanya. Orodhesha sifa ulizonazo zinazoendana na kazi unayoiomba.Mf. Kama ni mtu unayependa watoto, kupika, kuongea kiingereza au kuchapa katika kompyuta.

2. Ongezea Mdhamini

Huyu ni mtu muhimu ambaye mwajiri anaweza kuwasiliana naye ilikupata wasifu wako, anaweza kuwa mwajiri wako wa zamani, mwalimu, kocha au hata rafiki wa familia ambaye anafanya kazi katika tasnia sawa na unayoimba. Hakikisha ni watu wanaoweza kukuongelea vizuri kuhusu uwezo wako na ufanisi wako katika taaluma yako ama ubora wako katika kazi.

3. Ipangilie vizuri

Mpangilio unamaanisha maneno gani yatumike wapi ama yakae wapi hasa. Koza wino kwenye vichwa vya habari, pigia mstari taarifa muhimu na andika aya katika mpangilio unaolingana. Lakini pia unaweza kuandika kwa kuorodhesha uzoefu wako, elimu na ujuzi ulionao.

4. Tumia vitu sahihi

Tumia kalamu ya bluu na karatasi nyeupe hii itakufanya uonekane msomi. Kama utaamua kuandika kwa mkono basi hakikisha unatumia kalamu inayoandika vizuri na tumia rula kuchora mistari iliyonyooka, mpangilo mzuri wa muandiko hufanya barua ya wasifu kuwa na mvuto. Lakini muombe rafiki, au mwana familia au mwalimu ili akusadie kukagua uandishi.

5. Hakikisha unaihifadhi

Kama wasifu wako umechapwa kwa kompyuta hakikisha umeihifadhi vizuri. Kama unatumia kompyuta iliyopo shuleni au toka katika kompyuta ya eneo maalum hakikisha unajitumia CV yako kwenye barua pepe yako. Lakini pia ni jambo la maana sana kama utai ihifadhi kwenye flashi au hata kuiweka katika simu yako kama unavyoweka miziki na picha.

6. Sambaza Wasifu wako (CV)

Baada ya kumaliza kazi hii nzito. Ni muda wa kuisambaza sasa. Unaweza kutuma CV yako kupitia barua pepe au hata kwa sanduku la barua ili kuomba kazi iliyotangazwa, lakini kama inawezekana nenda kabisa katika maeneo unayotamani kufanyia kazi ama kutana na watu. waulize kama wanazo nafasi na kabidhi wasifu wako kwa mtu sahihi. Omba kuonana na afisa mwajiri kama inawezekana.

Na kwa sababu tayari umeshaandaa wasifu wako, toka kasake ajira. Kila la kheri.

Share your feedback