Unataka kufanya kazi gani ukiwa mkubwa?

Hizi hapa ni hatua 3 za kukusaidia namna ya kuanza

Mawazo yako (3)

Je Mara nyingi umekuwa ukiulizwa unataka kufanya kazi gani ukiwa mkubwa? Ahhh - linaweza kuwa swali la kufadhaisha ikiwa haujajua bado!

Usijali! Tunazo hatu 3 rahisi unaweza chukua kuanza safari ili kugundua njia yako. Ndiyo, ni safari, huwezi gundua kazi unayo taka kwa usiku mmoja tu. Kwa hivyo kuwa mvumilivu na anza kutafuta!

1. Zingatia unachofurahia kufanya

Je unapenda kuchora? Labda unaweza fikiria kuwa mchoraji. Je unafurahia kusimuliaa hadithi? Waandishi hugeuza usimulizi wa hadithi na kuifanya kuwa kazi. Au labda unafurahia hesabu na kutatua matatizo? Unaweza kuwa mfanyabiashara au mhasibu. Ndoto yako inafaa kuwa jambo unalofurahia kufanya - kwa hiyo fikiria hasa kuhusu unachopenda.

2. Fikiria kitu unachokiweza vizuri

Ni jambo Zuri sana kuwa na ujuzi wa kitu fulani. Hukusaidia kujenga ujasiri wako. Hivyo fikiria kipaji ulichonacho ambacho unatamani kukikuza zaidi. Je wewe ni bora katika michezo? Labda unaweza kuwa mwanamichezo mashuhuri. Je wewe ni bora katika kutatua matatizo? Wahandisi hutatua shida za watu! Je wanafunzi wenzio wanakufuata ili uwasaidia kufanya mazoezi ya darasani? Labda unaweza kuwa mwalimu.

3. Fikiri zaidi na gundua mambo mapya

Fungua macho yako na uone kazi zinazofanywa na watu wanakuzunguka. Unaweza ukagundua sekta mpya ambayo hukuwahi kufikiria hapo awali. Lakini pia kuna kozi nyingi unazoweza kujiunga baada ya kumaliza shule au kipindi cha likizo unaweza kuzijaribu pia. Unaweza kugundua kipaji kipya ambacho hukuwahi kudhani unacho.

Kuanza ndio jambo la muhimu. Ikiwa unajua tayari kazi unayotaka kufanya utakapokuwa mkubwa... Andamana nayo! Ifuate. Ikiwa bado haujui, usishtuke. Kama tulivyosema, hii ni safari na safari huchukua muda. Unaweza chukua barabara kadhaa tofauti, lakini ukifuata moyo wako utafika ulipotaka hatimaye.

Je umeshajua unataka kufanya kazi gani ukiwa mkubwa? Tuambie kuhusu ndoto zako na malengo yako kwenye sehemu ya maoni hapo chini.

Share your feedback

Mawazo yako

Uthubutu pia unahitajika. Siku zote tusiwaangalie walioshindwa wakati waliofanikiwa wapo.

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Ndoto Yangu Nikuwa Star Mkubwa Wa music Tanzania Africa

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Mfugaji Wa kuku

Machi 20, 2022, 8:25 p.m