Usijilaumu. Fanya kwa kadri unavyoweza.
Faiza, mwenye umri wa miaka 16 alivunjika moyo wakati duka la babake lilipofungwa na hakuwa na uwezo wa kulipa karo ya shule. Ingawa alikuwa na uwezo wa kujiandikisha kwa ajili ya mtihani wake wa mwisho, shule ilimwambia kuwa asingeweza kuendelea kuhudhuria na akajisikia mwenye kukata tamaa. Angewezaje kujisomea kwa ajili ya mtihani ikiwa asingeweza kwenda shule? Faiza alifadhaika na alikaribia kukata tamaa, mpaka wakati alipoona bango lilivutia macho yake alipokuwa akipita pembezoni mwa maktaba yake ya mtaani. Bango hilo lilikuwa la msichana mdogo aitwaye Malala. Alikuwa ameshika kitabu, na maelezo hapo chini yalisema:
”Hebu tuchukue vitabu vyetu na kalamu zetu. Ni silaha zetu zenye nguvu zaidi. Mtoto mmoja, mwalimu mmoja, kitabu kimoja na kalamu moja inaweza badilisha ulimwengu.”
Msichana yule katika bango lile alionekana jasiri na mwenye bidii, na wakati huu ndipo Faiza alitambua kwamba anaweza kuwa kama msichana huyu pia. Faiza alipenda kusoma na hakupaswa kukubali bahati mbaya ya babake kuharibu maisha yake ya usoni.
Mchana huo, Faiza alitembelea rafiki zake wawili wa karibu wa shuleni na kuwaambia wazo lake. Aliwauliza kama wangemfundisha walichojifunza shuleni kila alasiri. Kwa njia hiyo, marafiki zake wangeweza kupima uwezo wao, na yeye angeweza kujifunza mambo mapya.
Miezi michache iliyofuata ilikuwa migumu na kulikuwa na muda mwingi ambapo Faiza alijiuliza kama angeweza kuendelea. Hata hivyo, kila alasiri bila kukosa, Faiza alikutana na marafiki zake kwenye bustani na wasichana hawa walisoma. Watu walianza kuona jinsi wasichana wale walivyokuwa na bidii, na mwalimu wa mtaa huo aliyekuwa amestaafu alijitolea kumsaidia Faiza na maandalizi yake ya mtihani wa mwisho. Akivutiwa na kujitolea kwa Faiza na shauku yake ya kupata elimu.
Mtihani ulipokaribia, Faiza alianza kuogopa, lakini kila wakati sauti hiyo iliyomkatisha tamaa ilipomwambia kuwa hataweza, alikumbuka maneno ya msichana yule shujaa kwenye bango. Alipokumbuka maneno yale, aligundua kwamba alikuwa na uwezo wa kubadilisha ulimwengu wake.
Miezi michache baada ya mitihani yake, alipata barua aliyokuwa anaitumainia – aligundua kwamba alikuwa amefaulu mitihani yake. Faiza na familia yake walikuwa na furaha sana. Licha ya hali yake ngumu, Faiza alijiamini. Sasa ndoto yake ni kuwa mwalimu siku moja, na kuhimiza wasichana wengine wadogo kufuata ndoto zao.
Hadithi ya Faiza inatufundisha sisi Springsters kwamba ingawa wakati mwingine mambo hayaendi kulingana na mipango, na vikwazo, huonekana kutokea kusikojulikana lakini ni muhimu usijilaumu mwenyewe na ufanye kadiri uwezavyo.
Share your feedback