Nifuate njia ya nani

Wakati ambapo huna uhakika wa kusikiliza akili au moyo wako

Hakuna kitu kigumu kama kuhitajika kuchagua kati ya wazazi wetu na machaguo yetu binafsi. Labda, tulilala kwenye kitanda kimoja kwa miaka kumi na miwili na wazazi wetu (ndiyo, nililala kwenye chumba changu cha kulala nilipokuwa kwenye shule ya kati), kuishi kwenye nyumba moja nao, damu yao kutiririka kwenye mishipa yetu, lakini bado sisi ni watu tofauti. Tuna mawazo na moyo tofauti.

Sijawahi kuwaambia wazazi wangu kuhusu ndoto yangu ya kuwa mwandishi. Nilihitajika kusoma vichekesho na riwaya zangu kwa ujanja huku nikifanya hisabati na kabla ya kulala. Sasa, wananiomba kufanya kazi katika kampuni ya kimataifa yenye mshahara mkubwa na manufaa mengi. Hilo ndilo kosa langu la kutotaka kuwaambia wazazi wangu. Siwataki nyinyi wasichana kufanya kosa lilo hilo. Ningalikuwa nimewaambia wazazi wangu, huenda wangalininunulia vitabu na kunituma kwenye warsha za uandishi. Huenda wangalinisaidia. Huenda wangali.... Kutakuwepo na uwezekano mkubwa wakati wa kuzungumzia kitu ambacho hatukukifanya.

Ni kosa langu kuwa mbali na wazazi wangu. Nilijifunza mambo machache. Mawasiliano ni njia bora ya kwanza kujaribu kutatua tatizo. Kufuata njia yako binafsi si vibaya, isipokuwa kuishia kuwakwaza wazazi wako. Hivyo, zungumza nao, waza nao, na uwaonyeshe jitihada zako za kutimiza ndoto yako. Wana moyo, watakusikiliza. Ni binadamu, watakusikiliza. Ni wazazi wako, watakusikiliza. Lakini lazima pia utambue kwamba huenda wakawa na maoni tofauti nawe na huenda usikubaliane nao. Sikiliza kile watakachosema na huenda wakawa na jambo la maana.

Hata hivyo, fahamu kuwa wazazi wako wameishi muda mrefu zaidi yako na wanakupenda. Kwa hivyo ukijaribu kuzungumza nao na hawataki kukusikiliza jaribu kuelewa ni kwa nini wangependa mambo wanayokutakia na mjaribu kufanya uamuzi pamoja. Chaguo lako linapaswa kuwafanya kuteseka? Unaweza kufanya unachotaka kufanya kando? Angalia machaguo yako. Lakini, hakuna madhara, hivyo zungumza nao kwanza. Kudhani kabla ya kusikia maneno moja kwa moja kutoka kwenye kinywa cha wazazi wako kutakufanya tu kusumbuliwa na “ningali”.

Share your feedback