Jilinde
Baadhi ya mambo unayoweza kuyafanya
Kwa bahati mbaya, dunia yetu si salama kila wakati - haswa kwa wasichana na wanawake vijana. Unyanyasaji wa kingono unaweza kuwatokea wasichana nyumbani, shuleni, sokoni, kazini kwao, au mahali popote. Unatakiwa uwe tayari huku umejiandaa kukutana na hali kama hizi.
Hivi hapa ni baadhi ya vitu unavyoweza KUFANYA kukusaidia kujilinda:
- Epuka maeneo hatarishi: Iwapo unatambua sehemu unayoombwa kwenda inaweza kuwa na vitu vya kukuletea hatari za kimwili au nyinginezo - basi kama inawezekana jaribu kuepuka kwenda.
- Tembea ukiwa na marafiki:Kwenye maeneo ambayo si salama,tembea ukiwa na rafiki mmoja au zaidi - usiwe peke yako!
- Tafuta Mtu anaeaminika: Iwapo unajisikia kutokuwa salama katika sehemu fulani au nyakati fulani (Kama unapotembea kwenda au kurudi kutoka shule), na ni LAZIMA UENDE, basi mwombe mtu unayemwamini akusindikize..
- Kila wakati mjulishe mtu mwingine wakati /mahali unapokwenda na utakaporudi. Ikiwezekana, uwe na mtu wa kukupokea mahali unakoelekea. Kwa kufanya hivi,lolote likitokea, wengine watajua namna ya kuchukua hatua.
- USIWAFICHE watu wazima mambo yanapokutokea wewe binafsi au marafiki zako - na mara zote uwahimize kuhakikisha wameshugulikia tatizo na kuwa halijirudii tena!
- WEKA MPANGO: Tafuta mtu mzima anayeaminika unayeweza kumwendea tatizo
likitokea. Hakikisha kuwa unafahamu pa kumpata mtu huyu au namna ya kuwasiliana naye unapohitaji msaada. Bonga na marafiki zako wengine kuhusu kupata watu unaoweza kuwaamini na ili wawalinde..
Share your feedback