Namna ya kujilinda
Mpendwa Bi. Nai,
Nimekuwa Facebook kwa karibu miezi 4 sasa. Nina marafiki wengi sana. Wengi wao ni watu ambao sijawahi kukutana nao hata siku moja. Kuna Mwanaume mmoja ambaye ni mtu nimekuwa niki chati naye kwa muda mrefu, sasa hivi anaomba tukutane. Anasema mimi ni mrembo na anaamini ya kuwa tutaendana sana. Ninahofia kuwaambia marafiki au wazazi wangu kwa sababu watasema kuwa si salama kwangu. Me naona nimempata mume wangu wa maisha, na ninatamani sana nionane nae .Nifanye nini?
Ni mimi nilie njiapanda
Mpendwa ulie njiapanda,
Huu ni mchezo hatari sana kukutana na mtu ulie fahamiana nae tu mtandaoni . Ni rahisi kwa watu kujifanya kuwa kitu wasicho mtandaoni. Huezi kujua hata ikiwa picha na mambo wanayo posti mtandaoni kama ni ya kweli.
Huenda huwa unajisikia poa kuposti mambo yako binafsi (siri) chapchap mtandaoni kuliko unavyoweza ana kwa ana. Hii hukufanya kuwa rahisi kudanganywa au kuhadaiwa. Ikiwa umeanza kuwa na hisia na mtu uliyekutana naye mtandaoni, anaweza kukushawishi mkutane mahali pa usiri, ambapo anaweza kukutumia kwa manufaa yake au hata kukudhuru.
Kama wasemavyo wahenga Hakuna kitu cha Bure. Kwa hiyo ikiwa mtu unae wasiliana nae mtandaoni anakuahidi kitu kizuri cha kuvutia au anakusifia sana basi huyo ni wa kutiliwa mashaka.Wanaweza kuwa na maneno matamu kama asali lakini lengo lao ni kupata kitu kutoka kwako.Huyo Mvulana unayedhani unampenda sanaa anaweza kuwa mzee Fulani hivi ambae anatumia Intaneti kutongoza wasichana.
Ukiamua kukutana na mtu, hakikisha kuwa umeandamana na rafiki yako. Usijaribu kwenda peke yako. Kutana na mtu huyo kwenye eneo la umma lililo na watu wengi wanaoweza kukusaidia endapo ikihitajika. Usiingie katika gari binafsi au usafiri wa umma pamoja naye. Asitambue unapoishi. Na usikae peke yako ukiwa naye hadi uhakikishe kutoka kwa watu mtaani ya kuwa ni wanamfahamu kama alivyojimbulisha kwako na salama kuwa naye.
Kuwa Makini, Ninakujali
Bi. Nai!
Share your feedback