Dondoo muhimu kwa ajili ya wasichana
TAMBUA. Dunia imejawa na hali na watu hatarishi. Haupaswi kujawa na hofu muda wote ila unatakiwa kujua kuwa jamii yako sio mahala salama muda wote.
FAHAMU KUWA: Wafahamu watu ama maeneo yanayokufanya ujisikie kuwa na wasiwasi au kuogopa na panga kuyaepuka, hii itakusaidia kujilinda na kuzuia kitu chochote kibaya kisikutokee.
TATHIMINI: kama mtu atakufuata au kuanza kukueleza mambo mabaya, amua utakachosema na kutenda. Yapo mengi unayoweza kuyafanya kama vile kukabiliana nae na kumwambia aache kufanya hivyo, unaweza kuondoka haraka kutoka katika hilo eneo au omba msaada kutoka kwa watu wanaokuzunguka.
JIAMINI: Sema HAPANA! Iseme kwa sauti, na kwa uhakika, na mara Nyingi pale ambapo mtu atakuonea.
TENDA: Kama utahitajika kufanya hivyo, usiogope kufanya kitu ili kuzuia uonevu au kudhalilishwa. Unaweza kufanya chochote kile iwe ni kwa kukimbia au hata kumpiga mtu ili kujilinda. Kama upo katika maeneo yenye mkusanyiko wa watu, ni salama zaidi kukabiliana na mtu. Kama upo peke yako fikiri juu ya njia za kukimbia.
EPUKA. Jaribu Kadri uwezavyo kuwaepuka watu wanaokufanya usijisikie vizuri au kukutishia. Lakini pia epuka kwenda katika maeneo ambayo unajua ni hatarishi. Kuwaepuka watu na hali za aina hii ni moja ya njia nzuri sana za kubaki salama. Pia epuka kutembea mwenyewe au kutembea usiku.
TENGENEZA MPANGO. Tafuta mtu mzima unayemwamini ambaye unaweza kumfuata Mara zote mambo yanapokuendea vibaya. Hakikisha unajua mahali unapoweza kuwapata au namna ya kuweza kuwasiliana nao pale unapohitaji rafiki wa kuzungumza nae. Zungumza na marafiki zako namna mnayoweza kupata watu mtakaowaamini na muweze kusaidiana kubakia salama.
Share your feedback