Mambo 10 yanayowavutia Wavulana …

Yanawafaa wasichana pia.

Umewahi jiuliza vitu gani hasa wavulana wengi hupenda kuhusu wasichana? Utashangaa mno, lakini haya majibu ni muhimu kwa mabinti pia. Hivyo soma zaidi na utaelewa mambo yatakayokusaidia. Maana sio ya wavulana tuu

1). Wavulana hupenda wasichana wanaojiamini... lakini pia si unajua – mtu hujiskia poa yeye binafsi akijiamini na wasichana hupenda hivyo pia. Hivyo kuwa jasiri kwa manufaa yako mwenyewe. Sio kwa ajili ya wavulana – kuwa WEWE!

2). Wavulana hupenda wasichana ambao wanajua kusimamama na kujitetea na kutoa maoni yao kuhusu mambo mbalimbali…Lakini usijifanye unajua zaidi kuliko wao . Sauti za wasichana zinafaa kusikilizwa kama watu wengine. Hivo toa maoni na yasimamie.

10_things_boys_love_2.png

3).Wavulana hupenda wasichana ambao wanaweza kujiamulia mambo wenyewe... na siku zote mtu hujisikia poa sana kama anaweza kujiamulia mambo yake. Sisi mabinti tunapaswa tujisimamie haijalishi wengine wanasema au wanatufikiria nini. Maisha ni yako! #wanawakewenyeuwezo

4). Wavulana hupenda wasichana wajanja wenye akili... Kwani nani hamkubali mjanja au mtu mwenye akili? Ni vizuri kwenda shuleni na kujali masomo …lakini si kwamba ufanye kwa vile wavulana wanapenda, bali itakusaidia kufikia pale unapotaka kuwa! Na hicho ndicho cha muhimu!

10_things_boys_love_4.png

5). Wavulana hupenda wasichana ambao hutia moyo wengine... na wasichana mara nyingi huwa wanapenda kutia moyo wasichana wenzao . Kusaidia wengine na kujitoa kwa ajili ya marafiki zako ni kitu poa sana!

6). Wavulana hupenda Wasichana ambao ni wastahimilivu... hata wasichana hupenda kuwa wastahimilivu pia. Inabidi uamini unaweza kukabiliana na changamoto mbalimbali.#hakunamipaka

10_things_boys_love_6.png

7). Wavulana hupenda wasichana wanaoweza kushirikiana na wengine... na hata wasichana hupenda ivo pia, sababu kushirikiana ni kitu kwa kila mtu! Ushirikiano hurahisisha kufikia ndoto zetu. Mambo makubwa yanaweza tokea ikiwa wavulana na wasichana wanaweza kuamua kwa pamoja. Haya sasa fanyieni kazi hili.

8). Wavulana hupenda wasichana walio na msukumo wa kufikia ndoto zao... Hivyo hivyo kwa wasichana pia. Kwa hiyo usiogope kushindwa, jiamini na pigania ndoto zako!

10_things_boys_love_8.png

9). Wasichana hupenda Wasichana ambao wana mitazamo chanya... na kuwa na mitazamo chanya hutusaidia kuwa na nguvu na maendeleo kimaisha. Hata pale ambapo mambo magumu yanaweza kutokea maishani, wewe usiangalie ugumu. Usibaki tu katika kulalamika balii tafuta suluhisho.

10). Wavulana hupenda wasichana wanaojipenda… hapa pia tunapenda kuonyeshana upendo. Jifunze kuona uzuri ndani yako, sababu maisha yako yana kusudi! Maalumu.

10_things_boys_love_10.png

Hata kama haya ndiyo mambo wanayopenda wavulana, ni vitu ambavyo vinakufaa hata wewe mwenyewe pia SIO wavulana tu.

Hivyo dada – zingatia vile utakavyojijenga na kukua kwa manufaa yako mwenyewe na sio kwa sababu ya jinsi wengine wanavyokuwazia. Maana utakuja kufurahia sana baadaye.

Share your feedback