Tayari una kila kitu unachokihitaji
Karibu naingia mwaka wangu wa mwisho wa elimu ya sekondari. Natamani kuwa mhandisi umeme hivyo napaswa kuwa na alama za juu. Nina shauku kubwa mno ya kutimiza ndoto zangu.
Lakini hivi karibuni wazazi wangu waliniambia natakiwa kuacha shule na kuolewa na moja ya marafiki wa familia yetu. Wanafikiri ni jambo zuri katika maisha yangu ya baadae.
Napenda sana elimu yangu na sipo tayari kujihusisha na kuwa na familia. Natambua wananitakia mema, lakini ningeweza kuwaonyesha kwamba naweza kujenga maisha yangu mwenyewe pasipokuwa na mvulana.
Siku moja usiku niliwakalisha chini na kuwaeleza sababu 3 za kwanini sihitaji kuwa na mvulana katika maisha yangu kwa sasa.
Kuzingatia masomo yangu ndio msingi mkuu wa maisha yangu ya baadae. Niliwaambia wazazi wangu kuwa elimu pekee ndiyo ambayo inaweza kunihakikishia maisha yangu ya baadae. Niliwaonyesha alama nilizopata darasani na kuwaonyesha maoni ya baadhi ya waalimu jinsi walivyoniona mwenye akili sana darasani. Baba yangu alifurahi sana na alijawa na tabasamu usoni.
Pesa yangu, maamuzi yangu. Kipato nilichokuwa nikikipata kwenye kazi zangu za mwisho wa wiki kilinitosha kujilipia gharama za masomo na kuniruhusu kujifunza ujuzi mwingine. Masomo ya wiki nzima na kazi mwishoni mwa wiki hakutoi nafasi ya kuwa na mvulana. Naweza kusoma na kujiingizia pesa zangu mwenyewe, ambazo zitanifanya kuwa huru katika maisha yangu badala ya kuwa tegemezi kwa mvulana.
Wanawake jasiri ndio wa muhimu zaidi. Kupitia shule, nilijiunga kuwa mjumbe wa programu maalumu ya mafunzo chini ya wanasihi. Pale wanawake wanapohitimu masomo yao wanapatiwa msaada wa kutimiza malengo yao. Mnasihi wangu aitwae Farah amekuwa akinisaidia kujiandaa na maisha ya kesho. Yeye yupo chuoni anasomea kozi ya uhandisi na wakati huo huo anafanyakazi katika kampuni la umeme. Huwa ninamtembelea kazini na amekuwa akinifundisha vitu vingi. Kwa msaada wake Nina uhakika nitaweza kupata alama zitakazo niruhusu kusoma kozi ninayoitaka katika chuo kikuu.
Ninawashukuru wazazi wangu kwa kuyasikiliza mahitaji yangu. Sasa wananiunga mkono ili niweze kumaliza mwaka wangu wa mwisho na wananitia moyo kujiunga na chuo kikuu.
Share your feedback
Mawazo yako
Mimawazoyangunkwamba nimetamankuoamwanamuke wakujakufanyanaemaishamazuri katkamaishayangu
Machi 20, 2022, 8:25 p.m
Latest Reply
Apovp
AtaungekuWakamawemudada utaniambiajeaombatuwazo
Machi 20, 2022, 8:25 p.m
Latest Reply
Apovp